Tuesday, April 29, 2008

Uchaguzi Chuo Kikuu UDSM wadorora



Jackson Odoyo na Christopher Maregesi wa Mwananchi

KUTOKUWEPO kwa jina la mgombea urais wa serikali ya wanafunzi (DARUSO) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Odong’ Odwar raia wa Uganda aliyekuwa akikubalika na wanachuo walio wengi, baada ya jina lake kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho kwa madai kuwa hakuwa na sifa ya kuwa chuoni hapo kimesababisha wanafunzi wengi kususia uchaguzi huo.

Pamoja na wanafunzi wengi kususia uchaguzi ila wachache waliojitokeza kupiga kura waliongozwa na wasichana, huku wavulana wengi wakionekana kuvinjari sehemu mbalimbali katika vituo vya kupigia kura chuoni hapo bila kupiga kura.

Hata hivyo ilielezwa kuwa sababu kubwa iliyofanya wavinjari katika vituo hivyo ni kuwabainisha wenzao ambao walidhaniwa kuwa wangekaidi na kusaliti msimamo wao.

Mwitikio wa uchaguzi haukuwa mkubwa baada ya wapiga kura wengi kukataa kupiga kura kwa kile walichodai kuwa mgombea waliyekuwa wanamtaka hakuwepo hivyo hawakuwa na sababu ya kupiga kura kumchagua mtu asiye chaguo lao.

Hata hivyo kulikuwa na kampeni ya chinichini chuoni hapo iliyolenga kuzua wanafunzi kutopiga kura ingawa baadhi yao walionekana wakivinjari katika vituo vya kupigia kura bila kupiga kura. Kwa habari zaidi soma Mwananchi kesho.

No comments: