Friday, April 04, 2008

migodi yafuguliwa Mererani

Na Mussa Juma wa Mwananchi Mererani

SERIKALI imeruhusu shughuli za uchimbaji kuendelea katika migodi ya madini ya
Tanzanite ya Mererani wilayani Simanjiro katika maeneo ya kitalu C
kinachomilikiwa na wawekezaji wa Tanzanite One na kitalu D baada ya kufungwa
kutokana na maafa yaliyotokana mafuriko ya maji na kuuwa zaidi ya wachimbaji 64.

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Henry Shikifu alitangaza uamuzi huo jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari na wachimbaji katika kikao kilichofanyika kituo
cha polisi katika machimbo ya Tanzanite Mererani.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na Naibu waziri wa Nishati na madini,
Adam Malima, Shekifu hata hivyo alisema uchimbaji wa migodi katika eneo la kitalu
B utaendelea kufungwa hadi hapo kamati ya maafa itakaporidhika na kuopolewa miili
ya wachimbaji wadogo wote waliofariki na kukamilika kwa zoezi ya kuboresha migodi
mingine katika kitalu hicho.

Uamuzi huo, wa kufunguwa migodi ya kitalu C na D na kuendelea kuifunga migodi ya
kitalu B ambayo ndiyo imeathirika sana na maafa hayo kunatokana na mapendekezo ya
Rais Jakaya Kikwete alipotembelea migodi hiyo na kuitaka kamati ya maafa ya
kufanyatathimini na kuhakikisha katika kipindi cha siku tatu wanafungua migodi
hiyo.

Awali serikali ilitangaza kusitisha zoezi hilo Jumapili iliyopita kupitia kwa
Waziri wa Madini na Nishati William Ngeleja ili kupisha zoezi la kuopoa miili ya
wachimbaji waliokufa kwa mafuriko hayo.

Katika agizo lake Waziri Ngeleja alisema wanafunga migodi ili wachimbaji wote
waelekeze nguvu zao katika zoezi la kuokoa miili na maisha ya wenzao waliokumbwa
na maafa.
Post a Comment