Sunday, April 06, 2008

Mwandishi Mkongwe afariki dunia



Marehemu John Mndolwa

MWANDISHI Mwandamizi na Mratibu waHabari na Matukio wa televisheni yaITV na Radio One, John Mndolwa (46),amefariki dunia leo alfajiri majira ya saa 10 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa naMkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One, Joyce Mhaville, marehemu Mndolwa alilazwa hospitali ya Kairuki kwa wiki moja. Kifo chake kimesababishwa na shinikizo la damu.

Mndolwa ambaye alizaliwa Novemba 9,1962 mkoani Tanga alianza kazi za uandishi mwaka 1980 katika Idara ya Habari ya Radio Tanzania (RTD) na aliajiriwa na ITV na Radio One Julai 1994.
Mipango ya mazishi inaendelea kufanyika. soma zaidi habari hii ya kuhuzunisha kwa kwenda lukwangule.blogspot.com

Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu - AMINA/AMEN

No comments:

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...