Tabata Dampo mambo yao tambarare



TUME iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro, kuhakiki uhalali wa viwanja vya waathirika wa bomoabomoa ya Tabata Dampo kabla ya kulipwa fidia, imeanza kazi jana.

Akizungumza na wahanga hao jana, Mwenyekiti wa tume hiyo Michael Ole Mungaya alisema, utekelezaji wa zoezi hilo unakwenda sanjari na kupiga picha waathirika hao wakiwa wamesimama kwenye viwanja vyao.

Ole Mungaya alisema, Wanatarajia kazi hiyo itamalizika ndani ya siku mbili na waathirika watapatiwa barua maalum, zikiainisha uhalali wa umiliki wa nyumba kwa kuzingatia namba ya leseni za makazi na picha ya mmiliki halali wa kiwanja husika.

"Fedha zao zitakapoanza kutolewa, walipaji watakuwa na nakala za walipwaji... hivyo wakifika ofisini, fomu zao zitalinganishwa na zilizopo kwenye kumbukumbu zetu, kama kutakuwa hakuna shida watapatiwa hundi zao,"alisema Ole Mungaya.

Comments