Masikini mtoto azikwa


Mtoto aliyechinjwa alipewa sumu ya panya


WAKATI mwili wa mtoto, Salome Yohana (3) aliyefariki dunia kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili, umezikwa jana katika makaburi ya Tabata/Segerea kwa Bibi, Kaimu Kamishina wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Liberatus Barlow, amesema mtoto huyo alipewa sumu ya panya kabla ya kuchinjwa kichwa chake.

Kamishna Barlow alisema inasadikiwa mtoto huyo aliuawa kwa sumu kabla ya kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na Ramadhani Mussa (18) ambaye anadaiwa aliondoka nyumbani kwao Tabata akiwa na kisu, panga na sumu ya panya.

Alisema baada ya Ramadhani kufanya tukio hilo hakurudi tena nyumbani hadi alipokamatwa na polisi akiwa na kichwa cha mtoto.

Barlow alisema mtuhumiwa Ramadhani aliendelea kutozungumza, lakini alionyesha eneo alilofanya mauaji hayo, mita chache kutoka katika nyumba aliokuwa marehemu siku hiyo ya tikio.

Aliongeza kutokana na kauli ya mama mzazi wa mtuhumiwa, Khadija Ally na utata uliopo juu ya kifo cha mtoto huyo, vipimo zaidi vimechukuliwa na ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi wa kina. Habari hii ya Festo Polea.

Comments