Wednesday, August 15, 2007

Zitto Kabwe



Wachimbaji wadogo wa mgodi wa Mererani wametoa ahadi ya kumlipa mshahara na marupu rupu ya kipindi chote atakachokuwa amefungiwa wakati huo huo chama cha demokrasia na maendeleo Chadema leo mchana kimetoa tamko kupinga kufungiwa kwa mbunge wake Zitto Kabwe kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge kufuatia hoja yake binafsi kuhusu kusainiwa mkataba wa madini na Waziri Karamagi huko ughaibuni hivi karibuni.



Zitto mwenyewe amesema hakubali anakata rufaa, yapo mengi ya kujiuliza kabla ya kuchukua maamuzi kama haya. Moja kwanini Kabwe adanganye, na kama kweli kadanganya kwa maslahi ya nani, na kama Waziri ni mkweli kwanini anaogopa kuchunguzwa. Hivi Polisi halali wakija kwako na vibali halali wakasema ndani mwako kuna mali za wizi na wewe ukaamini kweli hakuna mali za wizi kwanini usikubali kukaguliwa ili usichafuliwe? Tujadili

1 comment:

Anonymous said...

Kuna jambo moja rahisi sana bunge na serikali wanatakiwa wafanye au tuwalazimishe wafanye:

1. Kabwe kasema mkataba ulisainiwa nje
2. Serikali na bunge vimekataa
3. Je tutajuaje yupi anasema ukweli kama sio uchunguzi wa wazi kufanywa? Hakuna jambo jingine zaidi ya hilo. Kama kuna pande mbili zinatoa taarifa zinakinzana, basi uchunguzi ufanywe tujue ukweli. Hakuna habari ya kuanza kutishia watu kwa kuwafungia sijui bunge. Bunge lile letu. Wanataka kufanya kama vile mali yao.