Monday, August 20, 2007

Nani kasema kwamba nyinyi wasafi?

WAVUJA Jasho bwana tuna staili zetu za maisha tofauti kabisa na nyinyi mnaojifanya mna uwezo mkubwa wa maisha, nasema mnajifanya mna uwezo mkubwa wa maisha sababu mnatudhulumu kile ambacho na sisi tulistahili kuwa nacho.

Ingekuwa ni halali yenu basi nasi tusingekuwa na budi kukubali na kuwasifieni kwa hicho mlicho nacho, japo kuna wachache mno wenye halali, lakini kwa mtizamo wetu wavuja jasho, tunajua hicho mlicho nacho aidha mmekiiba au kukidhulumu kutoka kwetu bila ya sisi kujua.

Ndiyo maana maisha yetu ni magumu yataendelea kuwa magumu kwasababu hata wanaojidai kuwa wana lengo la kutusaidia wanafanya hivyo ili kusudi wapate wingi wetu ili wakaombee misaada.

No comments:

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AMALIZA ZIARA YA SIKU MOJA MKOANI MBEYA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), leo ameondoka Mkoani Mbeya baada ya kukamilisha zi...