Saturday, August 18, 2007

Zitto Kabwe atikisa Dar





MAELFU ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo walijitokeza katika mapokezi na maandamano ya kumpokea Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe, (pichani) aliyesimamishwa ubunge hadi Januari mwakani.

Maandamano hayo, ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka kambi ya upinzani, yalianzia eneo la Ubungo, baada ya Zitto Kabwe kuwasili akitokea mjini Dodoma. Maandamano hayo yalipitia Barabara ya Morogoro na kuishia katika viwanja vya Jangwani ambako Kabwe alihutubia wananchi na kufafanua juu ya kile kilichotokea bungeni baada ya kuwasilisha hoja yake binafsi na baadaye kusimamishwa.

Katika hotuba yake kwa wananchi hao waliokusanyika Jangwani, Kabwe alisema iwapo mkataba wa madini wa mradi wa Buzwagi ungesainiwa nchini Uingereza ndani ya ubalozi wa Tanzania nchini humo, kusingekuwepo na tatizo. Picha hii ni ya Mpoki Bukuku.

No comments:

DKT. ABBASI AKAGUA MIRADI YA UTALII PORI LA AKIBA LA PANDE, ATOA MAAGIZO YA KUKAMILIKA KABLA YA AFCON 2027

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Julai 23, 2026, ametembelea Pori la Akiba la Pande jijini Dar es Salaa...