Monday, April 05, 2010

Beach party la thumni lafana Coco Beach


Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakikabidhi Thumni kwa Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando ambapo kila aliyekabidhi thumni moja alipewa zawadi ya vocha ya muda wa mawasiliano wa sh 10,000 wakati wa uzinduzi wa Tigo Thumni katika tamasha la Pasaka Beach Party lililofanyika Coco Beach jijini Dar wikiendi hii

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Faridi Kubanda ‘Fid Q’ akitumbuiza katika uzinduzi wa Tigo Thumni katika tamasha la Pasaka Beach Party ilofanyika Coco Beach jijini Dar wikiendi hii.
KWA HABARI ZA KINA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI HEBU TEMBELEA hapa

Friday, April 02, 2010

Wizi wa Simu


Askari wa usalama barabarani akimsindikiza jamaa aliyedaiwa kupora simu ya mkononi mjini Morogoro leo asubuhi.PHOTO/JUMA MTANDA

Ijumaa Kuu


Member of Catholic Church kisses a cross at Good Friday mass, held at Saint Joseph Cathedral Church in Dar es Salaam yesterday, to remember crucifying and death of Jesus Christ, more than 2000 years ago. PHOTO/EMMANUEL HERMAN

Ujumbe wa Tanzania Kwenye Mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU)


Spika wa Bunge Samuel sitta akitoa shukrani zake kwa Balozi Cisco Mtiro kwa mapokezi mazuri (kulia) kwa niaba ya ujumbe wa Tanzania unaohudhuria mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wakati wa chakula cha usiku jana,katika Hotel ya Conrad mjini Bangkok. Balozi Cisco licha ya kuwa Ubalozi wake upo Kuala Lumpar Malaysia, pia anashughulikia nchi ya Thailand ambapo kwa kipindi hiki cha mkutano wa 122 wa IPU naye yupo Bangkok kuratibu ugeni wa Tanzania katika nchi hii.

Spika wa Bunge Samuel Sitta na Balozi Sisco Mtiro wakibadilishana vitabu vilivyo tiwa sahihi za wajumbe waliohudhuria Mkutano wa 122 wa IPU toka Tanzania na wageni waalikwa kama ishara ya kumbukumbu ya mkutano huo. Picha na Afisa Habari wa Bunge Owen Mwandumbya

Rais Jakaya Kikwete apokea ujumbe kutoka Misri


Rais Jakaya Kikwete akipokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Misri Hosni Mubarak wa Misri toka kwa Mhe.Profesa Mohamed Nasr El-Deem Allam ambaye ni Waziri wa maji na Umwagiliaji wa Misri ikulu jijini Dar leo asubuhi. Picha Freddy Maro/ Ikulu

Thursday, April 01, 2010

Alhamis Kuu Zanzibar


MAPADRI WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA ZANZIBAR WAKIINGIA KANISANI KWA MAANDAMANO KUADHIMISHA MISA AMBAPO WALIRUDIA VIAPO VYAO MBELE YA ASKOFU WA JIMBO HILO AUGUSTINO SHAO KWENYE KANISA LA MTAKATIFU JOSEFU MJINI ZANZIBAR JANA.

ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA ZANZIBAR, AUGUSTINO SHAO AKITOA MAHUBIRI KWA WAUMINI WALIOHUDHURIA MISA YA KUWAOMBEA MAPADRI KWA KAZI YAO YA WITO ILIYOFANYIKA KWENYE KANISA LA MTAKATIFU JOSEFU MJINI ZANZIBAR JANA.
PICHA NA MARTIN KABEMBA.

Makamanda wa UVCCM


Kamanda mpya wa UVCCM Manispaa ya Moshi,Aggrey Marealle akimvisha kofia ya ukamanda wa UVCCM kata ya Karanga ,Thomas Mangia ambaye pia ni diwani wa kata hiyo.

Kamanda mpya wa UVCCM Manispaa ya Moshi,Aggrey Marealle akimvisha kofia ya ukamanda wa UVCCM kata ya Majengo diwani wa kata hiyo,Christopher Lyimo

Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Steven Kazidi akimvisha kofia ya ukamanda wa UVCCM Aggrey Marealle muda mfupi baada ya kusimikwa katika sherehe ambazo zilifanyika nje ya uwanja wa soko la pasua,Marealle pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...