Monday, May 03, 2010

JK: Sihitaji kura za wafanyakazi



RAIS Jakaya Kikwete leo ameushangaza umma wa Watanzania baada ya kuanza kukiuka misingi iliyokiunda Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuwaheshimu Wakulima na Wafanyakazi pale alipokutana na wazee wa MSkoa wa Dar es Salaam na kutoa hotuba kali akiwashutumu viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafabnyakazi Nchini (Tucta) kuwa ni wanafiki kwa kuendelea kushinikiza mgomo wa wafanyakazi licha ya mazungumzo yanayoendelea kati yao na Serikali.

“Hawa viongozi wa Tucta walisema sisi serikali ni watu wasioambilika… hawa viongozi wa Tucta ni waongo,” alisema Rais Kikwete akisisitiza kuwa hii ni moja ya sababu iliyomfanya jana awajibike kujibu.

“Sasa iweje tunakubaliana hili, kesho yake asubuhi unazungumza kama hatujakubaliana,” alisema Rais na kusisitiza: “Ninayo kila sababu kuhoji dhamira zao iwapo kweli wana nia thabiti ya kuwabeba wafanyakazi ama wana lao jambo.”

Kauli ya TUCTA

"Rais katumia lugha isiyo nzuri, hutuba yake imejaa vitisho na si demokrasia pia lugha aliyoitumia siyo nzuri na mbaya zaidi ametoa tamko lake bila ya kutusikiliza,"alisema Nicholaus Mgaya, Naibu Katibu Mkuu wa Tucta.

"Kwa muda wote tumekuwa tukijadili agenda tatu, kodi kwa wafanya kazi, maboresho ya mafao ya uzeeni na mishahara, lakini, Rais alizungumzia mishahara pekee jambo ambalo siyo haki,"alisema Mukoba na kuongeza:

"Kauli ya Rais Kikwete kwamba tulikubaliana kukutana Mei 8 mwaka huu kuzungumzia suala la mishahara, siyo ya kweli kwani hata taarifa ya Baraza la Majadiliano ya pamoja inaonyesha kuwa tulikubaliana kutokubaliana," alisema.

Watoto waliouawa wazikwa



MIILI ya watoto watatu waliouawa na mama yao mzazi kwa kukatwakatwa na shoka Alhamisi iliyopita imezikwa leo nyumbani kwao eneo la Kariwa kata ya Longuo B manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Taarifa iliyotolewa na baba mzazi wa watoto hao, Aloyce Thadei alisema kuwa ibada ya mazishi ya kuaga watoto hao itafanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya kaskazini usharika wa KCMC.

Thadei alisema watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali wanatarajiwa kuhudhuria msiba huo ambao ni wakuhuzunisha na kuwa tayari ndugu wa karibu waliokuwa wanasubiriwa tayari wameshafika.

Watoto waliouawa na mama yao ni Rose Thadei (12) ambaye ni mlemavu wa akili na viungo, Noel Thadei (5) na Antony Thadei (2).

Barabara kufungwa kwa saa tatu



Leo Mkuu wa Mkoa wa DSM William Lukuvi, ametangaza rasmi kufungwa kwa
barabara 3 muhimu kwa masaa machache mpaka mkutano wa World Economic Forum
uishe. barabara hizo ni Sam Nujoma, Nyerere na Bagamoyo Rd (Ali Mwinyi Rd)

Kufungwa barabara ya Bagamoyo ni kuhamishia watumiaji barabara hiyo Old
Bagamoyo road, sasa hivi tu kwa wale watumiaji wanakoma ubishi kwasababu
foleni ni masaa yote sasa hivi kutokana na miundo mbinu mibovu, sasa
wakiamishia watumiaji wengine wote si itakuwa balaa.

Anasema Mkuu wa mkoa kwamba ni kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa 3 na
kufngwa tena jioni saa tisa mpaka saa kumi na mbili jioni, sasa mimi
navyojua hii ndio pick hrs yenyewe, sasa si uchumi wote utasimama.

Mpira wa Olympiki






Mkurugenzi wa Taifa wa Olimpiki Maalumu, Frank Macha akiinua mpira wa Olimpiki utakaotumika kuzindua fainali za Kombe la Dunia 2010 zitakazoanza Juni 11 hadi Julai 11 mwaka huu Afrika Kusini, akiwa na wanaotembeza mpira huo katika nchi kadhaa duniani, Andrew Alis (wa pili kushoto) na Christian Wach. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DHL, Dlase de Souza. Mpira huo unaotoa ujumbe maalumu wa kuhimiza walemavu kushiriki michezo ya Olimpiki, uliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana ukitokea Arusha, kwa udhamini wa Shirika la Ndege la Precision Air, utakuwepo nchini kwa siku sita, na leo (Mei 4, 2010) utawekwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kwa ajili ya kushuhudiwa na wananchi. (PICHA NA MPIGA PICHA MAALUMU)

Sunday, May 02, 2010

Mkutano wa Afrika wa World Economic Forum waiva


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waandishi wa Habari May 2, 2010 baada ya kukagua maadalizi ya mapokezi ya wageni watakaoshiriki katika Mkutano wa World Economic Forum unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam kuanz a May 5, 2010 kwenye ukumbi wa Mlimani City utakapofanyia mkutano huo. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lymo na kushoto ni Mkurugenzi wa Afrika wa World Economic Forum, Catherine Tweedie. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TICAD Ministerial Follow meeting at AICC


President Jakaya Mrisho Kikwete and Japanese Minister for Foreign Affairs Katsuya Okada arrives at Arusha International Conference Centre for the opening ceremony of the 2nd TICAD Ministerial meeting this morning (photos by Freddy Maro)
A cross section of participants to the 2nd TICAD Ministerial Follow up meeting at AICC this morning during the opening ceremony.
Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Bernard Membe(centre) introduces to President Jakaya Kikwete Japan Minister for Foreign Affairs Katsuya Okada shorly after the President arrived at Arusha International Conference Centre(AICC) to open the second TICAD Ministerial Follow up meeting this morning.

Mafanikio ya teknolijia ya mawasiliano


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Iringa(Iringa Girls) wakianza kuzitumia kompyuta walizopewa na Mfuko wa Vodacom, Mfuko huo ulitoa Kompyuta 15 zenye thamani ya shilingi milioni 10.5 kwa shule hiyo hadi sasa umeshatoa kompyuta 313 kwa shule za sekondari 34 hapa nchini zenye thamani ya shilingi milioni 216.

Meneja wa Vodacom tawi la Iringa, Mnare Murungwa akimkabidhi kompyuta Mkuu wa Shule ya sekondari Wasichana ya Iringa(Iringa Girls) Mchome Ernest, anayeshuhudia ni Meneja wa Mfuko wa Vodacom Yesaya Mwakifulefule.Mfuko huo ulitoa Kompyuta 15 zenye thamani ya shilingi milioni 10.5 hadi sasa umeshatoa kompyuta 313 kwa shule za sekondari 34 hapa nchini zenye thamani ya Sh milioni 216.

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...