Thursday, November 26, 2026

RAIS SAMIA ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA KWA KILA MAMA NA MTOTO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha huduma bora za afya ya mama na mtoto zinawafikia wote kulingana na mahitaji yao, hususan katika maeneo yenye upungufu mkubwa wa huduma hizo.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Novemba 26, 2026, katika Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kisayansi kuhusu Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe, unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

“Hakika, hakuna anayeweza kupingana na ukweli huu, kwamba huduma bora za mama na mtoto zinapaswa kuwafikia wanawake na watoto kulingana na mahitaji yao, hasa katika maeneo yenye upungufu mkubwa wa huduma,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ameeleza kufurahishwa na kaulimbiu ya mkutano huo, inayosisitiza usawa katika upatikanaji wa huduma za afya ya mama na mtoto kupitia ugharamiaji endelevu, ubunifu katika kutatua changamoto na kuimarisha mifumo ya afya nchini.

Katika mkutano huo uliowakutanisha viongozi, wataalamu na wadau mbalimbali wa sekta ya afya, Rais Samia pia ametembelea mabanda ya maonesho ya huduma mbalimbali za afya ya uzazi, mama na mtoto.

#AfyaYaMamaNaMtoto #RaisSamia #AfyaKwaWote #Tanzania










No comments:

RAIS SAMIA ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA KWA KILA MAMA NA MTOTO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha huduma bora za afya ya mama na mtoto z...