Wednesday, November 04, 2026

TANZANIA NA UGANDA ZAIMARISHA USHIRIKIANO, MRADI WA BOMBA LA MAFUTA EACOP WAPEWA MSUKUMO MPYA!



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu ya Entebbe nchini Uganda yamejikita katika kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya mataifa hayo mawili, hususan katika utekelezaji wa mradi wa EACOP unaounganisha Hoima nchini Uganda na Chongoleani, Tanga nchini Tanzania.

Mradi huo ni hatua muhimu katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji katika sekta ya nishati, huku ukitarajiwa kufungua fursa za ajira, biashara na maendeleo kwa wananchi wa nchi zote mbili.

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais ameambatana na viongozi waandamizi wa Serikali, akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Marco Gaguti, pamoja na viongozi wa Wizara ya Nishati na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

EACOP si bomba la mafuta pekee, bali ni daraja la ushirikiano, uwekezaji na fursa mpya za kiuchumi kati ya Tanzania na Uganda!

No comments:

DKT. MWIGULU AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA DRC

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemkorasi ya Kongo (DRC), Judith Suminwa Tuluka na wamejadiliana n...