Wednesday, November 25, 2026

MSAJILI WA HAZINA AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA NEWREST

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, pamoja na uongozi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), wamefanya mazungumzo na ujumbe wa kampuni ya Newrest, ulioongozwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Olivier Sadran.

Mazungumzo hayo yalifanyika Jumanne, Novemba 17, 2026, wakati ujumbe huo ulipotembelea Ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umetoa fursa kwa pande hizo mbili kubadilishana mawazo na kuimarisha mahusiano ya kitaasisi, katika muktadha wa kukuza ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi.






No comments:

SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUKABILIANA NA MAAFA

Na Mwandishi wetu Dodoma Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), limeipatia Serikali ya Tanzania msaada wa vifaa vya...