Tuesday, November 24, 2026

𝑵𝑫𝑬𝑱𝑬𝑴𝑩𝑰 𝑨𝑲𝑨𝑮𝑼𝑨 𝑺𝑶𝑲𝑶 𝑳𝑨 𝑲𝑰𝑹𝑼𝑴𝑩𝑨, 𝑨𝑻𝑨𝑲𝑨 𝑴𝑰𝑪𝑯𝑨𝑵𝑮𝑶 𝒀𝑨 𝑵𝑺𝑺𝑭 𝒀𝑨 𝑾𝑨𝑭𝑨𝑵𝒀𝑨𝑲𝑨𝒁𝑰 𝑾𝑨 𝑴𝑹𝑨𝑫𝑰 𝑯𝑼𝑶 𝑰𝑾𝑨𝑺𝑰𝑳𝑰𝑺𝑯𝑾𝑬 𝑴𝑨𝑹𝑨 𝑴𝑶𝑱𝑨


Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo amekagua ujenzi wa Soko la Kirumba, Wilayani Ilemela, Jijini Mwanza, unaotekelezwa chini ya Mradi wa  Uendelezaji wa Miji Tanzania (TACTIC). Mradi huo wa Shilingi bilioni 14.7, unaojumuisha barabara ya kilomita 2.9 inayoelekea sokoni, umefikia asilimia 76.6 na unatarajiwa kukamilika Januari 2027.

Makamu wa Rais ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo, na kupongeza kwa usimamizi mzuri, ambapo amehimiza kuendelea kumsimamia mkandarasi kwa ufanisi bila kumbembeleza ili aweze kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Wakati huohuo; Mhe. Ndejembi amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CP Salum Hamduni kufuatilia na kuhakikisha  Mkandarasi anawasilisha makato yote ya NSSF wanayokatwa Wafanyakazi kila mwezi kwa mujibu wa Sheria, baada ya wafanyakazi kulalamika kukatwa fedha zao na makato yao kutofikishwa kwenye Mfuko wa NSSF kwa wakati.







No comments: