Thursday, January 08, 2026

VETA MOSHI YAZIDI KUNG’ARA KWA ELIMU AMALI

………………..

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Antony Kasore, amesema kuwa Chuo cha VETA Moshi kimeendelea kuwa mfano wa mafanikio ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini kwa kushirikiana moja kwa moja na viwanda na migodi ili kuhakikisha mafunzo yanayofundishwa yanahakisi mahitaji ya soko la ajira.  

‎Kasore alieleza kuwa ushirikiano huo unawawezesha vijana kupata fursa za ajira kwa haraka, kwani wanapomaliza mafunzo wanakuwa tayari na ujuzi unaohitajika na waajiri na kwamba chuo hicho kinajivunia kuona vijana wake wakipata nafasi za kazi nje ya nchi, ambapo wahitimu hao wamekuwa wanajivunia kupata ujuzi wa vitendo kutoka VETA, ambao umewasaidia kuinua uchumi wa familia zao na kuchangia pato la taifa.  

‎Chuo hicho pia kimekuwa kivutio kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Vijana kutoka Comoro, Congo, Rwanda na kwinguneko wamekuwa wakijiunga na chuo hicho kusomea fani mbalimbali, jambo linalothibitisha ubora wa mafunzo yanayotolewa. 

‎Aidha, amesema kuwa VETA imeweka mkakati wa kuhakikisha watu wenye mahitaji maalum wanajiunga na mafunzo ya ufundi stadi bila kulipa ada. Hatua hii inalenga kuwaonyesha jamii kuwa nao wana uwezo wa kushiriki kikamilifu katika kuinua uchumi wa taifa.




 

No comments:

WAZIRI MASAUNI ASHUHUDIA NUSU FAINALI YA KOMBE LA MAPINDUZI ZANZIBAR

Zanzibar — Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Yussuf Masauni , ameshuhudia mchezo wa kwanza wa nusu fain...