Saturday, January 17, 2026

TAGCO YAONGEZA TIJA KWA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI






Chama Cha Maafisa Mawasiliano ya Serikali Tanzania (TAGCO) kimeendelea kuimarisha uwezo wa kuwajengea maarifa mapya Maafisa Mawasiliano wa Serikali kutoka taasisi mbalimbali nchini, hususani katika nyenzo kuu ya mawasiliano hatua inayolenga kuhakikisha maafisa hao wanakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi .

Akizungumza katika mafunzo hayo,Mkufunzi na mtaalamu wa Mawasiliano , Michael Malya, amesema  lengo kuu la mafunzo hayo ni kujiweka sawa katika masuala ya mahusiano baina ya watu na serikali, ili kujenga uelewa wa pamoja, kuimarisha mawasiliano yenye tija, na kuongeza uwazi katika utekelezaji wa majukumu ya kila upande.

"“Nimefurahi kuwa miongoni mwa wakufunzi katika mafunzo haya ya Maafisa Habari, kwani yanatoa fursa muhimu ya kuimarisha uelewa wa masuala ya mawasiliano, matumizi ya teknolojia, pamoja na kujenga mahusiano bora kati ya wananchi na serikali,”Micheal Malya Amesema.

Washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kuboresha utendaji kazi wao, hasa katika kuwasiliana kwa haraka na kwa usahihi, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za serikali na wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki , Afisa mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini (LATRA) Said Pazzi, amesema kuwa miongoni mwa mambo aliyojifunza kupitia mafunzo hayo ni matumizi ya teknolojia katika kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kila siku ndani ya taasisi, hususan katika kurahisisha mawasiliano, kuongeza ufanisi wa kazi, na kuboresha utoaji wa taarifa kwa umma.

Aidha, Maafisa hao wameipongeza TAGCO kwa kuandaa mafunzo ambayo yamehitimishwa jana tarehe 16 Januari, 2026, wakieleza kuwa yamekuwa na mchango mkubwa katika kujengea uwezo Maafisa Habari na kuinua tasnia ya mawasiliano ya serikali nchini.

No comments:

KIKWETE ASEMA MFUKO WA UWEKEZAJI WA FAIDA WAKUA KWA KASI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wawekezaji wa Mfuko wa...