Saturday, January 17, 2026

DK.MIGIRO AKAGUA UJENZI JENGO LA OFISI ZA CCM MAKAO MAKUU JIJINI DODOMA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt.Asha-Rose Migiro akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu John Mongella,leo Januari 17,2027 amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Chama hicho katika eneo la NCC jijini Dodoma.






KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Bara, Ndugu John Mongella, leo Januari 17, 2027 amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya CCM katika eneo la NCC, jijini Dodoma.

Ukaguzi huu umefanyika ili kuhakikisha miradi ya ujenzi wa makao makuu inaendelea kwa mpangilio unaokidhi viwango vya ubora na muda uliowekwa. Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Migiro amesisitiza umuhimu wa mradi huu katika kuimarisha miundombinu ya chama na kuhakikisha kuwa Ofisi mpya za Makao Makuu zinakidhi mahitaji ya kisasa ya kiutendaji na kiusalama.

Aidha, amewataka watendaji wa mradi na wakandarasi kushirikiana kwa karibu, kuhakikisha kila hatua ya ujenzi inatekelezwa kwa ufanisi, ubora na kwa wakati. Ukaguzi huu umeonesha jitihada kubwa za timu ya ujenzi na utekelezaji unaoendelea kulingana na mpango wa mradi.

Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu pia wamezungumzia mikakati ya kuimarisha huduma ndani ya Ofisi ya Makao Makuu mara itakapokamilika, huku wakisisitiza kuwa mradi huu ni sehemu ya jitihada za CCM kuhakikisha mazingira bora ya utendaji na usimamizi wa chama.

No comments:

KIKWETE ASEMA MFUKO WA UWEKEZAJI WA FAIDA WAKUA KWA KASI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wawekezaji wa Mfuko wa...