Wawekezaji wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza nao kwenye Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa Mfuko huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Bw. Sephania Solomon (wa tatu kutoka kulia) akisubiri kumpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kabla ya Waziri huyo kufungua Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF jijini Dar es Salaam. Wengine ni Watendaji wa WHI.
Na. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora-Dar es Salaam
Tarehe: 17 Januari, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) ametoa wito kwa wasimamizi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) kujitangaza, kutoa elimu na kubuni njia bora zenye ushawishi ambazo zitawezesha mfuko kupata wawekezaji zaidi ambao watakuza mtaji.
Mhe. Kikwete ametoa wito huo Januari 17, 2026 wakati akifungua Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa Wawekezaji wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake, ameipongeza Bodi, Menejimenti na Watumishi wote wa WHI kwa kufanikisha ukuaji wa Mfuko na thamani ya kipande. Alifafanua kuwa hadi kufikia tarehe 30 Juni 2025, ukubwa wa Mfuko uliongezeka hadi kufikia Shilingi bilioni 43.99 sawa na ongezeko la asilimia 69 kutoka Shilingi bilioni 25.97 zilizonakiliwa kipindi kilichoishia Juni 2024.
Aliongeza kuwa, ongezeko hilo lilihusisha pia kuongezeka kwa thamani halisi ya kipande kilichoongezeka kwa shilingi 16.86 kutoka shilingi 115.812 hadi shilingi 132.6730 sawa na pato la asilimia 14.6 kwa mwaka.
“Leo tunapata fursa ya kupokea taarifa ya utendaji wa mfuko wetu, hivyo ninawasihi kama wawekezaji tujadili jinsi ya kuuboresha kupitia fursa zilizopo, tuweke mikakati ya kuongeza thamani ya uwekezaji wetu ili uwekezaji wetu uwe na manufaa” alisema Mhe. Kikwete.
Aidha, Mhe. Kikwete alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuthamini mchango wa mifuko ya uwekezaji kama Faida Fund katika kukuza uchumi, utamaduni wa kuwekeza na kuongeza ustawi wa wananchi.
Kwa upande mwingine, Waziri Kikwete amewahimiza Watumishi wa Umma kuchangamkia fursa hiyo ya kujiwekea akiba za kifedha ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kustaafu. Watumishi wa Umma wanaweza kuwekeza kwa dirisha la e-Wekeza kupitia makato katika mishahara yao kila mwezi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akifurahia jambo wakati akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Bw. Sephania Solomon (kulia) kabla ya Waziri huyo kufungua Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) jijini Dar es Salaam.Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakitoa huduma nje ya ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF wakati wa Mkutano wa tatu (3) wa Mwaka wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wawekezaji wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza nao kwenye Mkutano wa Tatu (3) wa Mwaka wa Mfuko huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF jijini Dar es Salaam.







No comments:
Post a Comment