Saturday, December 14, 2024

DR. KEDMON MAPANA ATEMBELEA BANDA LA NHC!






Leo, Katibu Mtendaji wa BASATA, Dr. Kedmon Mapana, ametembelea banda la National Housing Corporation (NHC) kwenye Tamasha la Kimataifa la Maendeleo ya Filamu na Sanaa linaloendelea viwanja vya Posta, Dar es Salaam! 🎬🏠

Dr. Mapana amepongeza juhudi za NHC katika kuboresha maisha ya Watanzania kupitia miradi ya makazi ya kisasa na fursa za uwekezaji. Amesisitiza pia jinsi sanaa na sekta ya ujenzi zinavyoweza kushirikiana kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa! 🌍💡

Njoo na wewe! Tembelea banda la NHC ujionee fursa za kumiliki nyumba bora, ofisi za kisasa, na maeneo ya kibiashara kwa gharama nafuu. Hii ni nafasi yako ya kutimiza ndoto zako za makazi bora!

📍 Viwanja vya Posta, Dar es Salaam

👉 #MaishaNiNyumba #NHCTanzania #TamashaLaSanaa #FursaZaMakazi #KujengaNdoto #InvestInYourFuture


No comments:

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefan...