Monday, December 23, 2024

WAZIRI KOMBO APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MWAKILISHI MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI

 







Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thatib Kombo amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bi. Susan Namondo katika Ofisi Ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam Desemba 23, 2024.

Akipokea nakala hizo Waziri Kombo amempongeza Bi Nomondo  kwa uteuzi aliuopata na amemuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi atakachokuwa nchini kuuwakilisha Umoja wa Mataifa.

Aidha, Mhe. Kombo ameushukuru Umoja wa Mataifa kwa mchango wake katika kuiwezesha Tanzania kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya Afrika ya mwaka 2063 kupitia Mfumo wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNSDCF) wa mwaka 2022-2027. 

Kwa upande wake Mwakilishi huyo Mkazi wa Umoja wa Mataifa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa mapokezzi mazuri na amehaidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania ili kuwezesha utekelezaji wenye matokeo mazuri wa malengo ya maendeleo endelevu nchini Tanzania.

No comments:

TARURA MUSOMA WAPONGEZWA UJENZI WA MIRADI KULINGANA NA THAMANI YA FEDHA

  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi amewapongeza wafanyakazi wa TARURA wilaya ya Musoma kwa kufanya kazi kwa weledi n...