NA MWANDISHI WETU
WATEJA
zaidi ya 700 kati ya 2000 wa msimu wa sita wa promosheni ya kuhamasisha
malipo na manunuzi kwa njia ya kadi inayoendeshwa na Benki ya NMB ‘NMB
MastaBata – La Kibabe,’ wameshajizolea kitita cha jumla cha zaidi ya Sh.
Mil. 76.4, kati ya zaidi ya Mil. 300 zinazoshindaniwa kupitia droo za
kila wiki.
NMB
MastaBata – La Kibabe ni kampeni inayochagiza matumizi yasiyo ya pesa
taslimu, ambako wateja wa NMB wanaotumia Kadi za MastaCard kuchanja
kulipia huduma kwa njia ya QR Code, PoS na NMB Pay by Link, ambapo benki
hiyo huwazawadia kila wiki, kila mwezi na ‘grand final’ itakayofanyika
Februari 12, 2025.
Idadi
hiyo ya washindi na kiasi hicho cha pesa walizoshinda, kimekuja baada
ya kufanyika kwa droo ya saba, iliyofanyika Ijumaa Desemba 27, kwenye
Ofisi za NMB Tawi la Tegeta, ambako Meneja wa Tawi, Bi. Magreth Lwiva,
alichezesha akisimamiwa na Pendo Mfuru kutoka Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania (GBT).
Akizungumza
kabla ya droo hiyo, Bi. Magreth alisema jumla ya washindi 2000
watajishindia zawadi mbalimbali zilizotengwa na benki hiyo zikiwa na
thamani ya Sh. Mil. 300 na kwamba kila wiki wateja 100 hujinyakulia
kiasi cha Sh. 100,000, huku wengine 40 wakishinda zawadi za papo hapo,
zikiwemo vocha za manunuzi ‘shopping challenge.’
“NMB
MastaBata pia hutoa zawadi za kila mwisho wa mwezi kwa miezi miwili,
ambako washindi 15 hujinyakulia Sh. 500,00 kila mmoja, washindi watano
hujishindia safari ya kutembelea Mguga za Wanyama za Mikumi na
Ngorongoro na wengine watano kujishindia pesa hadi Sh. Mil. 4 za ada zao
au watoto wao.
“Katika
droo ya mwisho yaani grand finale, wateja wetu sita watajishindia
tiketi za kusafiri Kwenda Dubai wao na weza wao, ambapo wataka huko kwa
siku tano kwenye Hoteli ya Nyota Tano, safari ambayo itagharamiwa kila
kitu na NMB,” alibainisha Bi. Magreth mbele ya Afisa wa Idara ya
Biashara ya Kadi NMB, Salehe Nkuruvi.
Kwa
upande wake, Bi. Pendo Mfuru kutoka GBT, alisema Bodi yake inaishukuru
NMB kwa namna inavyoendesha droo zake kwa uwazi na haki, huku akiwataka
wateja wa benki hiyo kuwa huru wanaposhiriki droo mbalimbali, kwani
inazingatia sheria, kanuni na miongozi wanayopewa na GBT.
“Niko
hapa kwa niaba ya GBT, uwepo wangu hapa unalenga kuhakikisha droo
inachezeshwa kwa kuzingatia vigezo na masharti yanayosimamia michezo
hii, ili kupata wateja kihalali, ambalo ndilo jukumu mama la taasisi
yetu. Hivyo tunawahakikishia wateja wa NMB kwamba, haki, vigezo na
masharti vinazingatiwa,” alisema.
Comments