Wednesday, December 11, 2024

BASHUNGWA APOKELEWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI – ZANZIBAR

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent L. Bashungwa (Mb) amewasili na kupokelewa katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mara baada ya kuapishwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 10 Disemba, 2024.




Na Enna Simioni

Mapokezi hayo yamefanyika katika Ofisi za Idara ya Uhamiaji Zanzibar na kuongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo (Mb), Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi, Menejimenti ya Wizara, Wakuu wa Vyombo Vya Usalama pamoja na Watumishi.

Akizungumza baada ya kupokelewa, Waziri Bashungwa amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini kumteua kuhudumu katika Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Aidha, Waziri Bashungwa ameeleza kuwa atatenga muda wa Kukutana na Idara, Vitengo, Vyombo Vya Ulinzi na Taasisi zote zilizo chini ya Wizara hiyo kupata taarifa ya Utendaji kazi, mafanikio pamoja na kupitia changamoto na kuweka mikakati ya kuzifanyia kazi.

“Nitapata fursa ya Kukaa na ninyi kuangalia katika majukumu, mnafanikiwa wapi, changamoto ziko wapi, jitihada zinazoendelea katika utatuzi wa changamoto na tufanyeje ili tuweze kushirikiana kutatua hizo changamoto” amesema Bashungwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo (Mb) amemkaribisha Waziri Bashungwa na kueleza kuwa dira ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kuwa Wizara ambayo itaifanya nchi kuwa na amani, utulivu na mahali ambapo sheria zinaheshimika.

Sillo ameeleza dhamira ya Wizara ni kulinda maisha na mali, kuwezesha na kudhibiti utokaji na uingiaji nchini kwa raia na wageni, kuwarekebisha wafungwa na kutoa huduma kwa wakimbizi waliopo nchini.


 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...