Wednesday, June 07, 2017

UPDATES MSIBA WA MAREHEMU BALOZI CISCO MTIRO, MAZISHI KUFANYIKA JUMATANO


Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro (pichani) ambaye amefariki dunia juzi asubuhi  katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa siku ya LEO JUMATANO, kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. Shaaban Kessy Mtambo


Bw. Mtambo alisema  kwamba mazishi ya mwanadiplomasia huyo yamepangwa kufanyika leo JUMATANO saa saba adhuhuri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 

 Msiba upo nyumbani kwa marehemu mikocheni B jijini Dar es salaam ambako ndugu, jamaa marafiki, majirani na waliofanya kazi na marehemu wamekuwa wakimiminika kutoa mkono wa pole.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huu.


Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - AMINA

No comments:

WIZARA YA AFYA YAOMBA SH. TRILIONI 1.8 BAJETI YA 2026/2027

  Wizara ya Afya imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi trilioni 1.8 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma z...