Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani) kuhusiana na zoezi la uchangiaji damu salama na kuipongeza Benki ya KCB kwa kushiriki katika zoezi hilo lililofanyika Makao Makuu ya benki hyo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akimpongeza mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya KCB Bi. Francisca Alphonce kwa kuwa mmoja wa watanzania waliojitokeza kuchangia damu salama
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (wapili kushoto) kwenye picha ya pamoja na sehemu ya timu ya menejimenti ya Benki ya KCB Tanzania na baadhi ya wakilishi kutoka wizarani. Timu ya menejimenti ya Benki ya KCB, Wapili kulia ni Bw. Cosmass Kimario, wakwanza kulia ni Bw. Masika Mukule, wakwanza kushoto ni Bi. Christine Manyenye, wakwanza kushoto juu ni Bi. Joyce Wiki Mwashigadi na watatu kulia juu ni Bw. Rojas Mdoe.
Wafanyakazi wa Benki ya KCB Bank Tanzania leo wamechangia damu. Hii ni katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uchangiaji damu (world blood donor day) ambayo itaadhimishwa dunia nzima jumatano wiki hii, tarehe 14 Juni.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo ambalo lilihudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Cosmas Kimario alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.
“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Afya, Elimu Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu” alisema Kimario.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa swala la kuchangia damu ni la muhimu sana kwani kuna wagonjywa wengi wenye hitaji la damu hivyo elimu juu ya uchangiaji damu salama ni muhimu kutolewa kwa jamii ili kuifanya jamii kuwa na uelewa mpana juu ya zoezi hilo.
“Tumeamua kuandaa uchangiaji wa damu ili kuisaidia serikali katika sekta ya Afya hususani katika kupunguza vifo vinavyotokana na upungufu wa damu” aliongeza Kimario.
Akizungumza katika zoezi hilo Waziri Ummy Mwalimu aliipongeza Benki ya KCB Tanzania kwa mchango wake huo na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano wa ukarimu wa Benki hiyo, akibainisha kwamba serikali inahitaji kubwa la damu hivyo inawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wengi zaidi kujitokeza kuchangia damu na kuokoa maisha kwa kuwa serikali haiwezi kufanikisha malengo peke yake.
“Nawapongeza sana Benki ya KCB kuwa wakwanza kuanzisha zoezi hili mwaka huu. Nawahimiza na wengine wajitokeze na waige mfano huu” alisema Waziri.
Zoezi hilo lilifanyika makao makuu ya ya Benki ya KCB, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Wakizungumza mara baada ya kuchangia damu kwa hiari baadhi ya wafanyakazi wa benki ya KCB wamesema kuwa zoezi hilo limeenda vizuri na kuwa suala la kuchangia damu ni lamsingi sana kwani wapo watu waliopungukiwa damu, wagonjwa na wanaopata ajali na kuhitaji damu.
Kwako wewe mtanzania jiulize kwanini usichangie damu kuokoa maisha ya watanzania wengine.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB wakishiriki zoezi la uchangiaji damu.
Comments