Wateja wa M-PESA waanza kunufaika na gawio la Tsh bilioni 7.9


Dar es Salaam, Wateja wa Vodacom Tanzania PLC  ambao ni watumiaji wa huduma ya kifedha ya M-Pesa wameanza kunufaika na gawio la shilingi bilioni 7.9.Gawio hilo limeanza kuwanufaisha jumla ya watumiaji milioni saba wa huduma ya M-Pesa nchi nzima.
Utoaji wa gawio unaendana na matakwa ya Benki kuu ya Tanzania. Hadi sasa Vodacom tayari imeshatoa jumla ya shilingi bilioni 80 kama gawio ambalo huhifadhiwa kwenye akaunti maalum ya M-Pesa Trust iliyopo kwenye benki za biashara hapa nchini.
Kabla ya gawio la sasa, jumla ya Tsh  bilioni 72 zilishagawiwa katika awamu tofauti tangu kampuni hii ianze utaratibu wa kutoa gawio Mwezi Disemba 2016. Utoaji wa gawio hufanyika kila baada ya miezi mitatu na gawio la sasa ni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka 2017.
Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa biashara ya mtandao wa kampuni hiyo,Sitoyo Lopokoiyit alisema “M-Pesa  inamwezesha kila mteja kupata huduma ya kifedha. Tunapojitahidi kumfikia kila Mtanzania, tunaendelea kutoa huduma bora na za kisasa zinazoziwezesha Serikali na biashara kufanya kazi pamoja na huku tukitoa faida nono kwa mawakala na wabia wetu,” alisema
Mkurugenzi huyo aliwaasa wateja ambao tayari wameanza kunufaika na  gawio hili kutumia fedha hizo kununua Ukarimu b

Comments