KATIBU MKUU MAENDELEO YA JAMII AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA DC WA MISUNGWI

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Samwel Sweda ( wa pili kulia) wakati alipomtembelea Ofisini kwake hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Samwel Sweda akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga(kulia) alipomtembelea Ofisini kwake hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Elliurd Mwaitekele(kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga(hayupo Pichani) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi hivi karibuni kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Bi Deodata Makani na Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi kutoka Wizara hiyo Bi. Martha Chuma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga(kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Elliurd Mwaitekele(kulia) wakati wakijadiliana jambo mara baada ya Katibu Mkuu huyo kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi hivi karibuni.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga(kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Juma Samwel Sweda(kulia) wakati wakijadiliana jambo mara baada ya Katibu Mkuu huyo kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya huyo hivi karibuni.Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Misungwi Mwanza

Comments