Tuesday, June 13, 2017

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO KATIKA ZIARA YA MAFUNZO NCHINI UFARANSA


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akikaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo katika ubalozi wetu uliopo jijini Paris. Mhe Gambo yupo katika ziara ya mafunzo nchini Ufaransa, ambapo pamoja na mafunzo hayo amekua akiutangaza mkoa wa Arusha kama kitovu cha utalii nchini Tanzania. 

Mhe Gambo, akiwa huko mefanya mazungumzo na Balozi Shelukindo, na kubadilishana mawazo ya namna ya kuvutia wananchi wa nchi hiyo kutembelea Tanzania. 

Ufaransa ni moja ya zinazoleta watalii wengi nchini Tanzania. Pamoja na mambo mengine  Mhe RC na Balozi wamejadiliana mambo ya Msingi ya kufanya ili kuongeza watalii kutoka Ufaransa kuja Arusha, kupata wawekezaji kutoka Ufaransa kuja Arusha pamoja na namna ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani humo, pamoja na kuanzisha tukio la kimataifa la kutangaza utalii mkoani Arusha kila mwaka.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kukaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo katika ubalozi wetu uliopo jijini Paris.
Post a Comment