RAIS DKT MAGUFULI AWAANDALIA FUTARI WANANCHI WA MKOA WA PWANI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kunawa na kisha kuchukua chakula jana Jumatano Juni 21, 2017  katika futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha ambayo ilihudhuriwa pia na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  pamoja na viongozi wengine wa dini, serikali, vyama na watoto wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali vya yatima mkoani humo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (wa pili kulia) akichukua chakula jana  Jumatano Juni 21, 2017 katika futali aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani futari katika Ikulu ndogo ya Kibaha ambayo ilihudhuriwa pia na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali pamoja na viongozi wengine wa dini, serikali, vyama na watoto wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali vya yatima mkoani humo.

 Kina mama wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaya Mhe. Asumpta Mshama wakichukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa neno la shukrani jana Jumatano Juni 21, 2017  wa waliohudhuria  futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  akizungumza machache na kuomba dua baada ya futari iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.

 Sehemu ya waalikwa wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  baada ya   futari iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 21 Juni, 2017 amefuturisha wananchi wa mkoa wa Pwani na kuwataka waumini wa dini ya Kiislam na madhehebu mengine kuendeleza umoja na mshikano uliopo kwa muda mrefu kwa lengo la kudumisha amani nchini.

Mhe. Rais Magufuli amesema anaungana na waumini wa dini ya Kiislamu nchini katika kumi la mwisho la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuwaombea kumaliza kwa amani ibada ya Funga ya Ramadhani ikiwa ni kutekeleza nguzo ya nne kati ya nguzo tano ya dini ya kiislam.

Amesema kwa mujibu wa dini ya Kiislamu ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni muhimu kwani ni njia sahihi ya kujirekebisha kuachana na matendo maovu yanayoweza kusababisha kutenda dhambi.

‘’Ramadhani ni ibada muhimu kwa Waislaam kwani ndio mwezi ambao huchoma dhambi zao na kutenda matendo mema hivyo ni muhimu kwa ndugu Waislaam kuendeleza yote mema ambayo wanafanya katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuliombea Taifa.’’

Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Aboubakar Zubeir Ali ametaka wananchi wa Tanzania bila kujali itikadi za kidini kuendelea kuliombea Taifa ili lizidi kuendelea kuwa na amani.
Nae Kaimu Sheikh wa mkoa wa Pwani Sheikh Hamisi Mtupa amemshukuru Rais Magufuli kwa ukarimu wake wa kuwaaandalia futari wananchi wa mkoa wa Pwani ikiwa ni pamoja na makundi maalum ya watoto yatima wa kituo cha Bulome Foundation cha mjini Kibaha mkoani Pwani. 

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kibaha, Pwani
21 Juni, 2017

Comments