Friday, August 31, 2007
Thursday, August 30, 2007
Uwanja wa Taifa
mechi itapigwa hapa
Sh 3,000 ya zamani, sasa ghorofani
MASHABIKI watakaotaka kuona mechi ya kirafiki baina ya Tanzania na Uganda kesho wametakiwa kuwa makini wakati wa kukata tiketi ili kujua maeneo wanayotaka kukaa na nambari za viti, huku wakikumbushwa kuwa wale waliokuwa wakilipia Sh 3,000 na kusota juani, sasa wataona mechi wakiwa juu ghorofani.
Mkurugenzi wa michezo, Henry Ramadhan aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa uwanja mpya, ambao unajulikana kwa muda kama Uwanja Mkuu wa Taifa wa Tanzania, umejengwa kwa njia ambayo itatoa nafasi kwa kila mtu kuona michezo vizuri kulingana na kiasi atakacholipia.
"Kama kule (uwanja wa zamani) mtu alikuwa anasimama wakati wote wa mchezo na kupigwa na jua, kwenye uwanja mpya atakaa ghorofani sehemu ya juu kabisa na hatadhurika na jua wala mvua," alisema mkurugenzi wa michezo, Henry Ramadhan wakati akiwaonyesha wahariri wa michezo utaratibu wa kuingia uwanjani hapo jana.
"Tena ajabu ni kwamba yule atakayelipia Sh 3,000 na kukaa juu kwenye viti vya kijani, karibu na eneo la VIP, ataona mpira vizuri kabisa sawa na yule aliyelipia Sh 30,000.
"Sasa hapa tuwape nini. Huyu wa 3,000 ni sawa kabisa na yule wa Jukwaa la Kijani la Uwanja wa Taifa. Hawa watakaolipia Sh 3,000 ni theluthi moja ya mashabiki wote watakaoingia uwanjani.
"Lakini naomba muwaambie kuwa wale wenye mshawasha wa kushangilia, basi wachague sehemu ya upinde (iliyo nyuma ya maeneo ya goli yenye viti vya rangi ya machungwa) kwa kuwa huko ndiko hasa kwa washangiliaji, hata vikundi vya ngoma vitakuwa huko."
Ramadhan aliwataka mashabiki kuwa makini kununua tiketi kulingana na sehemu wanazotaka kukaa na kuzisoma vizuri kujua milango watakayoingilia, akibainisha kuwa wale watakaoingia kupitia lango kuu ni wale tu ambao watakuwa na tiketi za VIP.
"Wale watakaokuwa hawaelewi vizuri, au wataenda sehemu ambazo si zao, watakutana na watu ambao wamepangwa kuwaelekeza," alisema. "Naomba tu wawe wastaarabu wakati watakapoelekezwa la sivyo watasaidiwa na wanausalama watakaokuwepo."
Monday, August 27, 2007
Neptune
Mazingira hayo unayapata wapi?
Sunday, August 26, 2007
Sia majuu hapa ni bongo hii hii
Tuesday, August 21, 2007
Zee la Nyeti ndani ya nyumba
Afrika Mashariki sarafu moja 2012
MARAIS wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) jana walikubaliana kuwa na sarafu moja na soko la pamoja kwa nchi za jumuiya hiyo ifikapo mwaka 2012.
Sambamba na uamuzi huo marais hao pia wamesogeza mbele uamuzi wa uharakishwaji wa kuanzishwa kwa Shirikisho la Afrika ya Mashariki.
Akisoma taarifa ya pamoja ya Marais hao mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao katika Hoteli ya Ngurdoto jana, Katibu Mkuu EAC, Balozi Juma Mwapachu alisema wakuu hao wamefikia maamuzi hayo kutokana na maoni yaliyotolewa na wananchi wa nchi hizo na pia kuingizwa kwa Rwanda na Burundi kwenye jumuiya hiyo. Bonyeza hapa usome habari hii kwa kina katika gazeti letu la Mwananchi
Monday, August 20, 2007
Nani kasema kwamba nyinyi wasafi?
Ingekuwa ni halali yenu basi nasi tusingekuwa na budi kukubali na kuwasifieni kwa hicho mlicho nacho, japo kuna wachache mno wenye halali, lakini kwa mtizamo wetu wavuja jasho, tunajua hicho mlicho nacho aidha mmekiiba au kukidhulumu kutoka kwetu bila ya sisi kujua.
Ndiyo maana maisha yetu ni magumu yataendelea kuwa magumu kwasababu hata wanaojidai kuwa wana lengo la kutusaidia wanafanya hivyo ili kusudi wapate wingi wetu ili wakaombee misaada.
Saturday, August 18, 2007
Zitto Kabwe atikisa Dar
MAELFU ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo walijitokeza katika mapokezi na maandamano ya kumpokea Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe, (pichani) aliyesimamishwa ubunge hadi Januari mwakani.
Maandamano hayo, ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka kambi ya upinzani, yalianzia eneo la Ubungo, baada ya Zitto Kabwe kuwasili akitokea mjini Dodoma. Maandamano hayo yalipitia Barabara ya Morogoro na kuishia katika viwanja vya Jangwani ambako Kabwe alihutubia wananchi na kufafanua juu ya kile kilichotokea bungeni baada ya kuwasilisha hoja yake binafsi na baadaye kusimamishwa.
Katika hotuba yake kwa wananchi hao waliokusanyika Jangwani, Kabwe alisema iwapo mkataba wa madini wa mradi wa Buzwagi ungesainiwa nchini Uingereza ndani ya ubalozi wa Tanzania nchini humo, kusingekuwepo na tatizo. Picha hii ni ya Mpoki Bukuku.
RICHARD BEZUIDENHOUT AKIWA HOME


Richard mwenyewe akiwa katika pozi la kawaida tuu

Richard akuwa na dadake

Katika harakati za harusi yake yuko na dadake pamoja na babake.
Bonyeza hapa utaona mapicha kibao ya familia yao yeye pamoja na dada na babake.
Thursday, August 16, 2007
Mtukufu Aga Khan

KIONGOZI wa kidini wa Jumuiya ya Ismailia duniani Imam Aga Khan ameleezea nia yake ya kutaka kujenga Chuo kikuu kipya hapa nchini.
Akizungumza na Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein jana Ikulu Jijini Dar es Salaam Imam Aga Khan alisema chuo hicho kitajengwa mkoani Arusha na kwamba kitakuwa cha aina yake katika Afrika kutokana na kuhusisha masomo ya taaluma muhimu pekee.
Mara baada ya ndege aina ya LX-PAK kutua katika viwanja hivyo kwenye saa 12:30 mlango ulifunguliwa na kisha kiongozi mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo ya Aga Khan aliingia ndani ya ndege hiyo kwa ajili ya kumuongoza Aga Khan aweze kushuka.
Mara baada ya kushuka, Aga Khan alipokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya ndani, Joseph Mungai.
Kisha wimbo maalumu wa jumuiya yao ulipigwa na Brass Bendi ya polisi na baada ya wimbo huo kiongozi huyo alipata fursa ya kuangalia ngoma ya asili yao, sarakasi pamoja na ngoma ya kimasai iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili yake.
Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo, Mungai alisema ujio wa kiongozi huyo ni kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya uimamu wake katika madhehebu ya kiismailia.
Mungai alisema, Aga Khan ameweza kuwa na ushirikiano mkubwa katika nyanja ya kimaendeleo hususani kwenye sekta ya Eimu na Tiba.
“Nataka niwahakikishieni kuwa katika hili la Elimu, shule ya kwanza ya wasichana iliyoko kule Zanzibar ilianzishwe na babu yake huyu Aga Khan, pia anaendelea na juhudi kubwa za kuendeleza Elimu katika taifa letu,” alisema Mungai. Mdau Mpoki Bukuku alikuwako huko na picha hii ni kwa hisani yake.
"Mafisi": Magari Yanayovuta Magari Mabovu Jijini Dar es Salaam
Katika mitaa yenye pilikapilika nyingi za Dar es Salaam, kuna magari maalumu yanayojulikana kama "mafisi" ambayo kazi yake ni kuvuta magari mabovu au yaliyoharibika barabarani. Ingawa mara kwa mara mamlaka zimejaribu kuyapiga marufuku, bado yanaendelea kuwa sehemu ya kawaida ya maisha ya jiji.
Mafisi ni Nini?
Mafisi ni magari yenye muonekano wa zamani, machakavu na mara nyingi yakiwa katika hali mbaya ya kiufundi. Magari haya hutumiwa kuvuta magari yaliyopata hitilafu barabarani, yakiwemo ya kifahari na ya gharama kubwa, jambo ambalo mara nyingi huvutia mshangao wa wapita njia.
Kwa Nini Yanaitwa "Mafisi"?
Jina hili linahusiana na sifa ya fisi halisi katika mazingira ya porini—wanyama wanaojulikana kwa kula mizoga au mabaki ya wanyama wengine. Vivyo hivyo, magari haya hutokea kwa haraka pale panapokuwa na gari lililoharibika, kama vile fisi wanavyojitokeza pale panapokuwa na mzoga.
Tabia na Changamoto za Mafisi
- Ubovu na Uchafu – Magari haya mara nyingi hayajashughulikiwa ipasavyo, yakiwa yamechakaa na mara nyingine hayana taa au vioo vilivyo salama.
- Kutokufuata Sheria za Usafiri – Mafisi mengi hayana vibali rasmi na mara nyingine madereva wake huendesha bila kufuata taratibu za usalama barabarani.
- Uhitaji wa Huduma – Pamoja na changamoto zake, mafisi yana umuhimu kwani yanasaidia magari yaliyopata hitilafu barabarani, hasa katika maeneo yasiyo na huduma rasmi za kuvuta magari.
Je, Kuna Mbadala wa Mafisi?
Kwa kawaida, huduma rasmi za uokoaji wa magari kama vile breakdown trucks zinapatikana, lakini gharama yake huwa kubwa. Hali hii huwafanya madereva wengi kukimbilia mafisi kwa sababu ni nafuu zaidi.
Ingawa magari haya yamepigwa marufuku mara kadhaa, bado yanaendelea kuonekana mitaani, yakitoa huduma kwa wale wanaokosa mbadala wa haraka na wa gharama nafuu. Mafisi ni sehemu ya taswira ya Dar es Salaam, yakibaki kuwa kielelezo cha changamoto na ubunifu wa maisha ya jiji hili lenye pilikapilika.
Wednesday, August 15, 2007
Timu ya Muafaka
Zitto Kabwe
Wachimbaji wadogo wa mgodi wa Mererani wametoa ahadi ya kumlipa mshahara na marupu rupu ya kipindi chote atakachokuwa amefungiwa wakati huo huo chama cha demokrasia na maendeleo Chadema leo mchana kimetoa tamko kupinga kufungiwa kwa mbunge wake Zitto Kabwe kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge kufuatia hoja yake binafsi kuhusu kusainiwa mkataba wa madini na Waziri Karamagi huko ughaibuni hivi karibuni.

Zitto mwenyewe amesema hakubali anakata rufaa, yapo mengi ya kujiuliza kabla ya kuchukua maamuzi kama haya. Moja kwanini Kabwe adanganye, na kama kweli kadanganya kwa maslahi ya nani, na kama Waziri ni mkweli kwanini anaogopa kuchunguzwa. Hivi Polisi halali wakija kwako na vibali halali wakasema ndani mwako kuna mali za wizi na wewe ukaamini kweli hakuna mali za wizi kwanini usikubali kukaguliwa ili usichafuliwe? Tujadili
Tuesday, August 14, 2007
Mutoto wa Moro
Monday, August 13, 2007
Kilwa Kivinje
Sunday, August 12, 2007
Mambo ya Lindi hayo
Magofu ya Kilwa: Urithi wa Historia na Kivutio Maarufu cha Utalii
Historia ni jambo lenye thamani kubwa, linaloakisi maisha ya zamani na maendeleo ya jamii mbalimbali. Miongoni mwa maeneo yenye historia tajiri na yanayovutia wageni ni Magofu ya Kilwa, yaliyopo katika mkoa wa Lindi, Tanzania. Magofu haya ni sehemu muhimu ya Urithi wa Dunia kama ilivyotambuliwa na UNESCO, yakionyesha athari kubwa za ustaarabu wa Kiswahili na uhusiano wa kihistoria kati ya Afrika na ulimwengu wa Kiarabu, Asia, na Ulaya.
Magofu haya ni masalia ya majengo ya kihistoria kutoka enzi za Dola ya Kilwa, ambayo iliwahi kuwa moja ya vituo vikubwa vya biashara katika Pwani ya Afrika Mashariki. Biashara ya dhahabu, pembe za ndovu, na bidhaa nyingine muhimu ilikuwa ikifanyika hapa, ikiwaunganisha wafanyabiashara wa Kiarabu, Wareno, na Waajemi na bara la Afrika.
Miongoni mwa maeneo maarufu ndani ya magofu haya ni Msikiti Mkubwa wa Kilwa, ambao ni moja ya misikiti kongwe zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara, pamoja na Kasri ya Husuni Kubwa, jengo lililowahi kuwa kasri la kifalme lenye usanifu wa kuvutia. Aidha, kuna mabaki ya Husuni Ndogo, ngome iliyotumika kwa ulinzi, na magofu ya makazi ya wafanyabiashara wa Kiarabu, ambayo bado yanatoa taswira ya maisha ya zamani katika mji huu wa kihistoria.
Magofu ya Kilwa siyo tu sehemu ya historia, bali pia ni kivutio muhimu cha utalii kinachovutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi. Watalii wanaokuja hapa hupata fursa ya kujifunza historia ya Kilwa, kushuhudia usanifu wa majengo ya zamani, na kujionea urithi wa kihistoria wa Tanzania.
Kutembelea Kilwa ni safari ya kipekee inayowawezesha wageni kusafiri nyuma katika historia na kuelewa jinsi biashara, utawala, na maisha ya jamii za pwani yalivyokuwa katika karne zilizopita. Hifadhi ya magofu haya ni jukumu letu sote ili kuhakikisha kizazi kijacho kinapata fursa ya kushuhudia utajiri huu wa kihistoria.
Wafanyakazi wamtikisa JK wampa siku 30
Katika kuonyesha kweli wamekereka na ahadi wanazodai hazitekelezeki wafanyakazi mkoani Dar es Salaam, wamempa siku 30 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Nestory Ngulla, kufikisha malalamiko yao kwa Rais Jakaya Kikwete na kurejeshewa majibu, kuhusu nyongeza duni ya mishahara, ili kuepusha hatua nyingine watakazotumia kudai mishahara.
Tamko hilo lilitolewa na wafanyakazi hao kupitia risala yao iliyosomwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha maandamano ya amani yaliyoandaliwa na vyama 18 vya wafanyakazi nchini kupinga kima cha chini cha mshahara wa serikali, kilichopitishwa na bunge hivi karibuni.
Baadhi ya vyama hivyo, ni pamoja na cha Walimu (CWT), Sekta ya Afya (Tughe), Migodi, Nishati, Ujenzi (Tamico), Serikali za Mitaa (Talgwu), Mabaharia (Tasu), Walinzi binafsi (Tupse), Mashambani (Tpawu), Shughuli za Meli (Dowuta), Mawasiliano (Tewuta), Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (Raawu), Waandishi wa Habari (TUJ) na Chodawu. Picha ya Mpoki Bukuku
Wapiga Debe: Wanaopiga Kelele Kurejesha Abiria Kwenye Daladala
Katika vituo vya mabasi jijini Dar es Salaam na miji mingine mikubwa nchini Tanzania, kuna kundi la vijana wanaofanya kazi inayojulikana kama "kupiga debe." Licha ya shughuli hii kupigwa marufuku mara kwa mara, bado inaendelea kuwa sehemu ya maisha ya usafiri wa umma.
Wapiga Debe ni Nani?
Wapiga debe ni watu wanaosaidia daladala kupata abiria kwa kupiga kelele kutangaza ruti ya gari, kuwashawishi watu kupanda, na wakati mwingine hata kuwavuta kwa nguvu kwenye gari. Kwa kazi hii, hupata ujira mdogo kutoka kwa makondakta au madereva wa daladala, mara nyingi kati ya shilingi mia chache hadi elfu kadhaa kwa siku kulingana na idadi ya abiria wanaopata.
Kwa Nini Wapiga Debe Wapo?
Licha ya kupigwa marufuku, wapiga debe bado wapo kwa sababu zifuatazo:
- Ushindani wa Daladala – Madereva na makondakta wanahitaji abiria haraka ili wapate faida, hivyo huajiri wapiga debe kusaidia kujaza gari.
- Ukosefu wa Ajira – Vijana wengi wanakosa ajira rasmi, na kazi ya kupiga debe inakuwa njia rahisi ya kupata kipato, hata kama ni kidogo.
- Utaratibu Dhaifu wa Usimamizi – Ingawa mamlaka za usafiri zimejaribu kuwaondoa, utekelezaji wa marufuku haujawa wa kudumu.
Changamoto Zinazohusiana na Wapiga Debe
- Usumbufu kwa Abiria – Wapiga debe mara nyingi huwasukuma au kuwavuta abiria kwa nguvu, jambo linalowakera wengi.
- Uhalifu na Utapeli – Baadhi yao wanahusishwa na wizi wa fedha na simu za abiria, hasa katika vituo vyenye msongamano.
- Kero kwa Mamlaka – Wakati mwingine hupiga kelele na kusababisha fujo katika vituo vya mabasi, kuvuruga utaratibu wa usafiri wa umma.
Je, Kuna Suluhisho?
Ili kukomesha tatizo la wapiga debe, mamlaka zinapaswa:
- Kuboresha Mfumo wa Usafiri wa Umma – Mfumo rasmi wa kupanga daladala na kuzuia ushindani holela unaweza kupunguza hitaji la wapiga debe.
- Kuimarisha Utekelezaji wa Sheria – Wapiga debe waliosababisha usumbufu wanapaswa kuchukuliwa hatua madhubuti ili kuzuia shughuli hiyo.
- Kutoa Ajira Mbadala – Vijana hawa wangepata fursa za kazi nyingine, tatizo hili lingepungua kwa kiasi kikubwa.
Ingawa wapiga debe wamepigwa marufuku mara nyingi, bado ni sehemu ya maisha ya usafiri katika miji mingi ya Tanzania. Swali kuu linabaki: Je, tatizo ni wapiga debe wenyewe au ni mfumo wa usafiri na ajira unaowalazimisha kuendelea kuwepo?
Babu Aelezea Safari Yake ya Maisha: Kuelekea Kizazi Kipya Cha Vijana Wenye Umri Mdogo

Babu huyu ambaye amefika umri mkubwa, ameishi maisha ya kujitahidi na kupambana na magumu mengi katika kila hatua ya maisha yake. Akiwa ameona na kupitia kila aina ya changamoto, babu huyu amejivunia kusimama imara hadi kufikia umri huu. Amekutana na mambo mengi, lakini ameweza kushinda vikwazo vingi na kuendelea kuwa mzee mwenye hekima.
Katika kipindi cha maisha yake, amepitia magumu, lakini alijifunza kuwa maisha ni safari ndefu na lazima apambane ili kufika alipo sasa. Ametoa mifano ya maisha ya zamani na vile vijana wanavyohitaji kujituma kwa bidii kwa ajili ya mustakabali wao.
Kwa upande mwingine, mabadiliko ya kijamii na hali ya maisha yanavyoendelea kubadilika, ni dhahiri kuwa vijana wa sasa wanakutana na changamoto tofauti na wale wa zamani. Vijana wenye miaka 33 katika miaka 10 ijayo, wataonekana kuwa na maisha ya haraka, na wakati mwingine wanakuwa na mtindo wa maisha unaowafanya kuonekana kama "babu" kwa haraka. Hali hii inatoa funzo kwa vijana kuwa maisha hayaendeshwi kwa haraka na lazima kuwepo na juhudi ili kufikia mafanikio ya kudumu.
Safari ya maisha inahitaji uvumilivu na bidii kwa vijana.
JIJI LA DODOMA?????

Wednesday, August 08, 2007
Tuesday, August 07, 2007
Mshiriki wa Tanzania ana aibu
Suala hili linamfanya aanze kuonekana kama mtu anayeboa kuliko wote ndani ya nyumba, hata Watanzania nadhani wanaweza kuchoshwa na hali hii inabidi abadilike. Anatajwa mara chache mno na umaarufu wake miongoni mwa wenzie uko chini.
Katika siku yao ya pili, alfajiri mameti wa jumba la Big Brother wanaonekana kuondokewa na ujasiri waliokuwa nao siku ya jana walipokuwa wakiingia ndani ya jumba hilo, sababu Big Brother tayari keshawapiga mkwara mzito.
Wakati wa kuoga asubuhi ya leo kuna mambo kadhaa yalichomoza kuhusiana na joto la maji ya kuoga. Mameti wanagundua haraka kwamba kuna ujanja alioucheza Big Brother.
Meryl kwa mara nyingine tena anafanya kituko anavua nguo na kubakia mtupu, katika tukio hilo anafuatiwa na Tatiana, ambaye anaonekana kujawa na aibu tele kuonyesha mwili wake.
Pamoja na kuinyesha utundu na mara kadhaa kuwa karibu sana na wanaume,
, Lerato anaamua kuoga na nguo yake. Inawezekana hii ni mbinu yake ya kuwatia kiu mashabiki wake ili kusudi wawe na uchu wa kuona mwili wake.
Monday, August 06, 2007
Mshiriki wa Big Brother 2 mtanzania huyu hapa


Kama akishinda donge nono la dola za Marekani 100 000, Mtanzania, Richard Buzidenhout anasema atazitumia kununua vifaa vya kupigia picha za filamu . Mwakilishi huyo wa Big Brother kutoka Tanzania, mwenye umri wa miaka 24 na mwanafunzi wa fani ya filamu ana matarajio makubwa ya kuwa mtaalamu mahiri katika fani ya filamu na binafsi anamhusudu sana mtengenezaji filamu, Peter Jackson kwa umahiri wake.
Richard ambaye ni mshiriki pekee wa shindano hilo aliyeoa anasema kuwa anatamani sana kutembelea nyumbani kwao mkewe huko nchini Canada katika mji wa Brandon uliopo katika jimbo la Manitoba, Canada kushuhudia sehemu aliyokulia mkewe.
Anajielezea kama mtu anayependa mzaha, na kwamba ni mgumu sana kukasirishwa, lakini anasema tabia yake moja inayokera ni usumbufu na kelele nyakati za alfajiri, kabla wengi hawajaamka.
Anapanga kushinda Shindano hilo la Big Brother Africa 2 bila kushusha hadhi yake. Anapenda mazingira asili ya Afrika Mashariki, anasema kitu kinachomvutia zaidi ni kuendesha gari kupitia kreta ya Ngorogoro huku akishuhudia wanyama pori mbalimbali.
Pia anasema eneo analolihusudu kulitembelea ni Serengeti na maeneo ya Pwani hasa Zanzibar.
Tafadhalini Watanzania tumpigieni kura Richard ili aweze kushinda kitita na hatimaye kupandisha chati Tanzania kimataifa.
Bonyeza hapa au Bonyeza hapa
Ukitaka kumuona cheki Richard hebu Bonyeza hapa
wengine wanaoshiriki Big Brother Africa ni hawa

Bertha Miaka: 28 Nchi: Zimbabwe Mji anaotoka: Harare Kazi: Mwanasheria/mshauri wa Uhusiano na mawasiliano.

Code Sangala Miaka: 31 Nchi: Mali Mji anaotoka: Blantyre Kazi: Mtangazaji/ DJ

Jina Jeff Miaka: 23 Nchi: Kenya Mji anaotoka: Kisumu Kazi: mtunzi wa vitabu, mshauri na mjasiliamali

Justice Motlhabani Miaka: 23 Nchi: Botswana Mji anaotoka: Serowe Kazi: Mwandishi wa kujitegemea/Mwanafunzi

Kwaku Miaka: 30 Nchi: Ghana mji anaotoka: Kumawu Kazi: Mjasiliamali.

Lerato Miaka: 23 Nchi: Afrika Kusini Mji anaotoka: Soweto Kazi: Mratibu wa matukio

Maureen Miaka: 27 Nchi: Uganda Mji anaotoka: Entebbe Kazi: Mbunifu wa mitindo

Maxwell Miaka: 26 Nchi: Zambia Mji anaotoka: Lusaka Kazi: Opareta wa simu

Meryl Miaka: 21 Nchi: Namibia Mji anaotoka: Windhoek Kazi: Mhudumu wa Mapokezi

Ofunnekama Miaka: 29 Nchi: Nigeria Mji anaotoka: Lagos Kazi: Katibu Muhtasi.

Tatiana Miaka: 26 Nchi: Angola Mji anaotoka: Luanda Kazi: Msanii/mwanamitindo
Sunday, August 05, 2007
Olga Zarubina awa Miss Tourism Queen International 2007

Kwa maana hiyo Mrembo wetu Sophia Kapama kaambulia patupu, lakini si mbaya amejitahidi saana dada yetu tumpongeze.
Hebu cheki hapa.
Bonyeza hapa au hapaupate taarifa kwa kina zaidi. Utakuta mambo kama haya. Good thing is that by the time, I was writing this entry, I found the official announcement about winner of Miss Tourism Queen International 2007 in its official website.
In the official website of Miss Tourism Queen International, I could find that Olga Zarubina is 24 years old and her height is 1.78 meter. So, you can imagine that she is very tall. Well, I don’t think that she is beautiful but my opinion does not matter. The funniest thing is that there is absolutely no information about Olga Zarubina except that she is a model. I wonder what kind of model she is!
The picture that I have given her has been taken from the official website of Miss Tourism Queen International 2007.

If you want to see Olga Zarubina’s picture then you should visit the following entry:
Miss Russia is Miss Tourism Queen International 2007!
Wednesday, August 01, 2007
Mlima Oldonyo Lengai unavyoonekana sasa
Mama anafikiria nini?
*WATAFITI WA MIMEA VAMIZI WATUA SERENGETI
Na Sixmund Begashe - Serengeti Ziara ya kikazi ya watafiti wa mimea vamizi kutoka Jamhuri ya Cuba walioungana na wataalam wa ikolojia kutok...

-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
(Picha na Yahya Charahani) Kwa wale waliokulia maeneo haya, hili ni jambo la kawaida ukitoka mjini, shambani sijui hadi wapi kote ni haya h...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...