Bonde la mpunga

mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha mafuriko huku bonde la mpunga lilipo jengo la May Fair Plaza.

Comments

mwandani said…
Unajua tatizo la bonde la mpunga ni kuwa maji yote ya mvua yanayoelekea baharini hiyo ndiyo njia yake.

Ukiangalia mbele kidogo - ukipita kituo cha ccm kisiwani - utakuta daraja la kijitonyama - hicho kijito kina daraja dogo sana,mifereji kutoka mayfair imejaa udongo, maji hayaendi halafu kijito chenyewe hakiwezi kuhimili maji yote. Ukienda mbele kwa mwalimu maji yote yanashukia huko, halafu hakuna mifereji.

Zamani palikuwa na mifereji iliyokuwa na nafasi, maji ya mvua bonde la mpunga yalikuwa kama kiama. Mvua zikkisha tatizo mchanga ulioletwa na mvua - kuna watu walikuwa wakifyatua matofali kwa mchanga wa mvua tu.

Anyway, wakazi wa bonde la mpunga inabidi tuchukue hatua, japo tuchimbe mifereji mbele ya nyumba tu,na kwenye barabara kuu vifusi tuviondoe kwenye mifereji.
Ndesanjo Macha said…
Unaona mafuriko haya yametokea mwaka huu, usishangae yakitokea tena mwaka ujao, na mwaka ujao, na mwaka ujao. Utamaduni wa kutatua tatizo likishatokea au kabla ya kutokea hatujauzoea. Na sio kuwa hatujauzoea kwakuwa hatuwezi ila kwakuwa wenye wajibu huo hawajali na wananchi hawajui jinsi ya kutumia nguvu walizonazo kuwafanya wajali. Au kutumia nguvu zao kutatua tatizo wenyewe kama alivyopendekeza Mwandani.
nice good sharing information