Thursday, November 12, 2009

Flaviana Matata ndani ya New York



Flaviana Matata with Russell Simmons at Tuesday night's show. Flaviana Matata (born 1987) is a beauty queen who won the very first edition of the Miss Universe Tanzania pageant in 2007, and went on to represent her country in the Miss Universe pageant the same year, where she placed among the Top 15 semifinalists and ended up in 6th place after the evening gown competition. She was the first contestant from Tanzania to compete at Miss Universe, and compete with a shaved head.

Elizabeth wa BBA awasili na kuzungumza


Mshiriki wa Big Brother E,izabeth Gupta akiongea na wanahabari leo hoteli ya Paradise jijini Dar. Kulia ni bosi wa operesheni wa MultiChoice Baraka Shelukindo na shoto ni afisa operesheni wa MultiChoice Grace Urassa. Pamoja na mambo mengine Elizabeth amewashukuru wadau kwa kumpigia kura na kumpa taffu katika kipindi chote alichokuwa mjengoni.

Kasema ana mpango wa kurudi masomoni kwani ndio kwanza kamaliza kidato cha sita hivyo ana kiu ya kusoma sanaa na kuigiza pamoja. amesema anapenda kuigiza na kuimba na ameshawahi kuwa mtangazaji. amesema anatafuta sponsa kujiendeleza katika sanaa na akimkosa atajilipia mwenyewe.



Mshiriki wa Bigbrother Africa Revolution Elizabeth Gupta aliyewasili jana uwanja wa ndege wa mwalimu J.K.Nyerere akitokea sauzi.

Ugawaji samaki wa Magufuli wakwama



UGAWAJI wa tani 296.32 za samaki waliovuliwa kwa njia haramu katika ukanda wa Tanzania kwenye Bahari ya Hindi uliopangwa kufanyika jana, umekwama.

Samaki hao maarufu kama 'Samaki wa Magufuli', hawakugawiwa jana kwa taasisi zilizoteuliwa kupata mgawo kwa sababu ambazo hazikuwekwa bayana.

Kazi ya kugawa samaki hao ilipangwa kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kiwanda cha kuhifadhia samaki cha Bahari Foods kilichopo Mwenge.

Hata hivyo, utata uligubika kazi hiyo na kuifanya ishindiane na serikali haikutoa ufafanuzi kuhusu kukwama kwa zoezi hilo.

Majira ya saa 4.00 waandishi wa habari na baadhi ya wananchi walifika katika kiwanda cha Bahari Foods wakisubiri zoezi la ugawaji wa samaki hao lianze, lakini muda ulipita bila matumaini ya kuwaona samaki hao zaidi ya taarifa kutoka kwa walinzi wa kiwanda hicho kueleza kuwa zoezi hilo limesitishwa hadi litakapopangiwa siku nyingine.

Juhudi za kuwapata viongozi wa ngazi za juu akiwemo Waziri John Magufuli, katibu wa rasilimali za bahari, Gefrey Nanyalo, na viongozi wengine hazikuweza kufanikiwa.

Baadhi ya maafisa wa wizara hiyo, ambao kwenye majengo ya ofisi za wizara hiyo, walisema hawakuwa na taarifa rasmi kuhusu zoezi hilo zaidi ya kudai kutakiwa kusubiri taarifa kutoka ngazi za juu yao.

Walisema taarifa walizonazo juu ya kusitishwa zoezi hilo ambazo si rasmi ni kwamba wizara ilikosa vifaa vya kukatia samaki hao, lakini wadau walihoji sababu za wizara kutangaza zoezi hilo bila ya maandalizi.

“Mimi mwenyewe nilijua leo tunakwenda kwenye ugawaji samaki lakini muda si mrefu ndiyo nimepokea taarifa zikinieleza kuwa zoezi limesitishwa na litapangiwa muda mwingine, lakini sababu zaidi bado hazijatolewa ingawa za awali nimeelezwa kuwa ukosefu wa vifaa mbalimbali vya kukatia samaki hao ndiyo umekwamisha zoezi hilo,’’ alisema mmoja wa maafisa wa wizara hiyo. Imeandikwa na Festo Polea na Tumsifu Sanga.

Wednesday, November 11, 2009

Jina la Waziri Msolla latumika kutapeli


Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Peter Msolla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Msolla alikuwa akitoa taarifa juu ya matapeli wanaopigia watu simu kwa watu na kujigeuza sauti zao kufanana na yakwake ili wafanya utapeli wao. Picha na Peres Mwangoka.

WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msolla amesema amedhalilishwa na kuchafuliwa jina lake katika jamii baada matapeli kulitumia jina lake katika kufanya utapeli kwa njia ya simu.

Profesa Msolla aliyasema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kuhusu utapeli kwa njia ya simu kwa kutumia majina ya watu maarufu nchini.

Alisema yeye mwenyewe ameshaathirika na utapeli huo baada ya matapeli hao kutumia jina lake kufanya utapeli huo kwa watu mbalimbali.

Akielezea utapeli huo Profesa Msolla alisema matapeli hao wamekuwa wakiiga sauti yake na kuwapigia watu wakijitambulisha kuwa ni yeye(Msolla) na kwamba ana shida na anaomba kiasi fulani cha pesa.

“Hivi karibuni kumezuka utapeli ambapo watu wanaiga sauti ya mtu na kuzungumza kama ndio mhusika mwenyewe asilia kisha huonesha kuwa ana shida na anahitaji msaada hivyo huomba fedha kutoka kwa watu mbalimbali na kuwaelekeza zitumwe kwenye akaunti za benki mbalimbali hapa nchini;

Young boy down the street


Young boy sleep along Bibi Titi Road in Dar es Salaam yesterday, which is risk for his life PHOTO/FIDELIS FELIX

Tamko la Wazanzibari majuu

TAMKO LA MUWAZA KUHUSU KUKUTANA KWA :
RAIS AMANI ABEID KARUME NA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD
MUWAZA UMEFURAHISHWA KWA MSIMAMO WA VIONGOZI HAO WAWILI NA KUPONGEZA KWAO:
KUTETEA MUSTAKBAL WA ZANZIBAR
KUWAUNGANISHA WAZANZIBARI WAWE KITU KIMOJA
KUONDOSHA UHASAMA BAINA YA WAZANZIBARI
KUWASHAJIISHA WAZANZIBARI KWA PAMOJA KULETA MANDELEO ZANZIBAR
MUWAZA INAUNGA MKONO KWA KUTETEWA KWA NCHI, TAIFA NA DOLA LA ZANZIBAR
KUTETEWA MASLAHI YA KIUCHUMI YAKIWEMO MAFUTA YA ZANZIBAR
KULETA MAENDELEO YA KIJAMII - SIHA, ELIMU NA UTAMADUNI WA ZANZIBAR
KUTETEA HAKI ZA KIDEMOKRASIA BILA YA KUJALI ITIKADI PAMOJA NA KURUHUSU KILA MZANZIBARI KUWA NA UHURU WA KUPIGA KURA
KUTETEA MIHIMILI HALALI YA UTAWALA YA ZANZIBAR
KUREJESHA CHEO CHA MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR
KUREJESHA MAMBO ASILI KUMI NA MOJA YA MUUNGANO NA HATIMAE KUYAJADILI UPYA
KULIPA BARAZA LA WAWAKILISHI HESHIMA SAWA NA BUNGE LA MUUNGANO.
Dr. Yussuf s. Salim Mwenyekiti wa Muda
Copenhagen Denmark
yussuf_salim@hotmail.com

Zaidi ya watu 20 wapoteza maisha kwa kuangukiwa na mlima

MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana wilayani Same, imeleta maafa makubwa baada ya watu 30 kuhofiwa kufa kufuatia kitongoji chao kuporomokewa na mlima ambao ulizifunika kabisa nyumba zao wakiwa usingizini.

Kazi ya ukoaji ambayo ilikuwa ikifanywa kwa kutumia vifaa duni yakiwemo majembe ilikuwa ikiendelea ambapo hadi kufikia jana saa 9:00 mchana, miili ya watu 16 ilikuwa imeopolewa kutoka katika vifusi vya mlima huo ulioporomoka.

Mkuu wa wilaya ya Same, Ibrahim Marwa alisema kuwa hadi kufikia saa 9:30 alasiri, idadi ya maiti waliokuwa wameopolewa ni 16 na kulikuwa na majeruhi nane waliookolewa katika jitihada zilizofanywa na wananchi waliofika mapema eneo la tukio.

“Kwa takwimu ambazo tumepata ni kwamba idadi ya waliokufa inaweza kufikia 25 hivi japo hatuna uhakika lakini wapo majeruhi tisa ambao wanahudumiwa hapa hapa na timu ya madaktari na wataalamu wa Afya kutoka Same,”alisema mkuu huyo wa wilaya.

Alifafanua kuwa chanzo cha maafa hayo ni mvua nyingi zilizonyesha mfululizo kwa siku tatu na kufanya mlima huo kushindwa kuhimili na kuporomokea nyumba saba za wananchi wa kitongoji hicho na kuzifunika kabisa wakati wamelala.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mamba Miamba kulipotokea maafa hayo, Michael Chikira Mauya aliliambia Mwananchi kutoka eneo la tukio kuwa inakadiriwa nyumba hizo zilizofunikwa zinakadiriwa kuwa na familia za watu kati ya 20 na 28.

“Mpaka sasa hivi (saa 6:00 mchana jana) tumefanikiwa kutoa miili 12 na tunakadiria katika nyumba saba zilizofunikwa kunaweza kuwe na watu hadi 28 hivi…kwa kweli ni tukio ambalo ni baya sana hapa kijijini”alisema Diwani Mauya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, maofisa wengine wa polisi na askari wa vyeo vya chini na pia mkuu wa wilaya ya Same, Ibrahim Marwa walikuwa katika hekaheka za kuopoa miili ya waliokufa kutokana na janga hilo.

Tukio hilo limekuja wakati mvua ambayo imenyesha kwa siku tatu mfululizo katika kata za Maore, Ndungu, Kihurio, Bendera ikiwa imesababisha maafa makubwa na kusababisha vifo vya wanafunzi wawili ambao walisombwa na maji.

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...