Monday, October 06, 2008

Burdaani


Mwanamuziki kutoka Kenya, Nyota Ndogo akimpagawisha mmoja wa mashabiki waliohudhuria uzinduzi wa tamasha la Fiesta lililofanyika Uwanja wa Mkwwani tanga mwishoni mwa wiki

Sunday, October 05, 2008

Mabalozi wapo Tarime


picha ya kwanza ni Mkuu wa kikosi maalum cha operation, Venance Toss akiwa pamoja na
mkuu wa kikosi cha kuzuwia fujo(FFU) Anavlet Trasphery wakiwa wanawapokea mabalozi,
Janet Siddall wa Canada,Philip Parham wa Uingereza na Staffan Herrtrom wa Sweeden
ambao walifika jana Tarime kujionea hali ya kampeni hasa kutokana na kupata taarifa
za vurugu na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi. picha na mussa juma.

Vifaa hivyo mshindwe wenyewe


NMB’s Senior Marketing and Communication Manager Imani Kajura (first left) hands a jersey to Taifa Stars captain Henry Joseph as TFF general secretary Frederick Mwakalebela looks on. The bank handed equipment worth Tsh5.5million to the team which is preparing a World Cup qualifier against Cape Verde on Saturday.

Mambo yameiva Tarime


Pichani ni baadhi ya wapiga kura wakitazama majina yao katika vituo vya kupigia kura katika jimbo la Tarime baada ya kubandikwa jana. Picha na Mussa Juma.

Friday, October 03, 2008

Dada wa wangwe awaka



MALUMBANO baina ya ndugu wa aliyekuwa mbunge wa Tarime kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Marehemu Chacha Wangwe, yamezidi kupamba moto baada ya dada wa mbunge huyo kuibuka na kumkana mke mdogo, Doto Mohamed kuwa hatambuliki kwenye ukoo.

Kuibuka kwa dada wa mbunge huyo, Mary Zakayo Wangwe kumekuja siku mbili baada ya mke Dotto, ambaye alidai kuwa ndiye aliyeshirikiana na Wangwe hadi kupata ubunge, kupinga madai ya mke mwingine mdogo kuwa Chadema imeitelekeza familia ya marehemu, akisema kuwa ni mapema mno kuzungumzia hilo.

Mariam alikuwa wa kwanza katika malumbano hayo baada ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita na kuzungumzia mambo mengi kuhusu utata wa kifo cha mbunge huyo akilitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi zaidi, lakini akamwaga lawama kwa Chadema, jambo ambalo limezua malumbano baina ya wake hao na dhidi ya viongozi wa chama hicho, hasa katibu mkuu, Wilbroad Slaa.

Akizungumza na gazeti hili jana kijijini Kemakorere, dada huyo, Mary Zakayo Wangwe alisema kuwa Dotto Mohamed si mke halali wa Marehemu Wangwe kwa kuwa walishatengana na kwamba aliwahi kumshitaki Ustawi wa Jamii akidai apewe mali, lakini akashindwa katika kesi hiyo.

Wednesday, October 01, 2008

hivi ungekuwa wewe ungeacha kusaini??

Rais Kikwete

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na waumini wenzake katika Sala ya Iddi katika msikiti wa Kinondoni Muslim leo asubuhi.Rais Kikwete alirejea nchini jana usiku akitokea nchini Marekani ambapo alilihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa(The Un Generalk Assembly).

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...