Wednesday, April 12, 2017

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA TANO CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongoza kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Mbunge wa Mwibara(CCM) Mhe. Kangi Lugola akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Fakharia Shomar Khamis (CCM) akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mh. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Mbunge wa Ukonga (CHADEMA) Mwita Waitara akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Kilimo Uvuvi na Ufugaji Mhe. William Ole Nasha akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Mbunge wa Urambo (CCM) Magreth Sitta akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mhe. Peter Msigwa akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi Mhe. Stella Manyanya akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Mbunge wa Shaurimoyo (CCM), Mattar Ali Salum akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bungela Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira kazi na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama(kushoto) wakati wa kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma katikati ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia wambura(Kushoto) na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi Mhe. Stella Manyanya wakifuatilia kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 
Wajumbe nane kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia shughuli za kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. 

Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma. 

………………. 

SERIKALI YAFAFANUA KUSHAMIRI KWA BIASHARA YA VYUMA CHAKAVU, MPANGO WA KUUNDA BODI MPYA YA TUMBAKU NA UTENGAJI ASILIMIA MAALUM KWA WANAFUNZI KUTOKA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR 


Dodoma,Jumanne, 11 April, 2017. 

Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu kushamiri kwa Biashara ya vyuma chakavu,Mpango wa kuunda bodi mpya ya Tumbaku na Utengaji wa asilimia maalum kwa wanafunzi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, Ufafanuzi huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma. 


Kushamiri kwa Biashara ya Vyuma Chakavu 

Serikali imesema kuwa, imekwishaandaa Rasimu ya Muswada wa Sheria itakayoweka bayana taratibu na mfumo wa usimamizi na udhibiti wa biashara ya chuma chakavu katika hatua mbalimbali za uzalishaji,ukusanyaji,usambazaji,uuzaji na uyeyushaji wake kwa kuzingatia uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa manufaa ya Taifa. 

Hatua hiyo imekuja baada ya kuongezeka kwa mahitaji ya vyuma chakavu hapa nchini na duniani kwa ujumla na kubainisha maeneo yaliyoathirika sana kuwa ni mifumo ya kusafirisha Umeme,Reli na Barabara. 

Akifafanua kuhusu hoja hiyo, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage amesema Muswada huo umeweka bayana adhabu itakayotolewa kwa mtu atakayebainika kuharibu miundombinu. 

Aidha Mhe.Mwijage ametoa wito kwa Wananchi wote kutoa taarifa pindi waonapo mtu anayehujumu miundombinu kwa namna yoyote ile. 


Mpango wa kuunda Bodi mpya ya Tumbaku. 

Serikali imesema kuwa, iko katika maandalizi ya kuunda Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Tumbaku haraka iwezekanavyo na Wananchi watajulishwa kupitia tamko la Serikali mara baada ya taratibu kukamilika. 

Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha amesema kuwa, Serukali ilivunja Bodi ya Tumbaku kwa lengo la kufanya maboresho katika utendaji kazi wake. 

Ameongeza kuwa, hatua ya kuvunja Bodi hiyo haihusiani na kusitisha shughuli zinazotekelezwa katika Kilimo cha Tumbaku kwani wapo wataalamu wanaondeleza utekelezaji wa mpango uliopo wa kuendeleza zao la Tumbaku nchini. 

Aidha kwa kuzingatia kuwa wakulima wanahitaji huduma muda wote hasa kipindi hiki cha kuelekea masoko ya tumbaku kwa msimu wa 2017/18,Serikali kupitia mrajis wa vyama vya Ushirika nchini imeshateua timu nyingine ambayo ipo Mkoani Tabora ikiendelea kuratibu na kusimamia masuala mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuandaa upatikanaji wa pembejeo kwa msimu ujao. 
Serikali kuendelea kutenga fedha kwa wahitaji wa Mikopo ya Elimu ya juu. 
Serikali imesema kuwa itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu kwa kuzingatia Sheria,kanuni na taratibu na miongozo itolewayo mara kwa mara na serikali kupitia bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu. 
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Stella Manyanya amesema kuwa utoaji wa Mikopo unazingatia muombaji awe raia wa Tanzania,muhitaji,mlemavu au yatima na mabaye amedahiliwa katika elimu ya juu na mwenye kuchukua programu za vipaumbele vya Taifa kama Sayansi, Hisabati,uhandisi wa Gesi na Mafuta, Sayansi za Afya na Sayansi za Kilimo na Maji. 
Aidha Mhe.Manyanya amesema kuwa katika Mwaka wa 2015/16 Serikali ilitoa kiasi cha Tsh.bilioni 480 kugharamia Mikopo pamoja na ruzuku kwa wanafunzi wapatao 124,358. 

Ameongeza kuwa Serikali inalifanyia kazi suala la wanafunzi kutopata Mikopo ili kuongeza idadi ya wanafunzi. 

Imetolewa na: 

Idara ya Habari-MAELEZO.

No comments: