Thursday, April 13, 2017

WAZIRI LUKUVI AZINDUA BODI MPYA YA WAKURUGENZI WA NHC AKIIAGIZA IZINGATIE MASLAHI YA TAIFA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) uliofanyika leo mchana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kulia ni Subira Mchumo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya NHC na kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) uliofanywa leo mchana na Waziri Lukuvi. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akimuongoza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi kuingia ukumbini wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) uliofanywa leo mchana na Waziri Lukuvi. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dk Moses Kusiluka na Meneja wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano Kasibi Saguya kuingia ukumbini wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) uliofanywa leo mchana na Waziri Lukuvi. 

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe akizungumza kutoa maelekezo ya utendaji kazi kwa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa NHC wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). 
Kutoka kushoto, Wakurugenzi Raymond Mdolwa, Haikamen Mlekio, Fatma Chillo, Hamad Abdallah na Felix Maagi wakifuatilia hotuba ya Waziri Lukuvi wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe akizungumza na wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu katika picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Blandina Nyoni makao makuu ya NHC  leo.
 Wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC na Menejimenti ya NHC pamoja na Waziri wakiwa katika picha ya pamoja.
 Wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC na Menejimenti ya NHC pamoja na Waziri wakiwa katika picha ya pamoja.

Mwandishi Wetu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi ameiagiza Bodi Mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa kulisimamia Shirika kuhakikisha kuwa linajikita katika misingi yake iliyolianzisha kwa kuendeleza kwa kasi ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini kote huku likiendelea kujenga nyumba zingine kwaajili ya kuziuza kwa Watanzania na kuwawezesha wengi zaidi kuwa na makazi bora.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo kwenye Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC PLACE leo mchana kwa kuitaka Bodi hiyo ilisimaie Shirika hilo kwa maslahi ya Taifa huku ikihakikisha kuwa halipati hasara.

"Nataka NHC ijenge nyumba kwaajili ya watu masikini  kwa bei na ubora, mbuni mikakati yenye kuzingatia hili ili watanzania wengi zaidi waweze kumiliki nyumba bora. Simamieni misingi. bodi mpate muda wa kuwasikiliza wapangaji. Ujenzi wa nyumba gharama nafuu uongeze kasi mfafanue suala hili katika sera yenu kila mtu ajue nyumba ya gharama nafuu maana yake nini,"alisema.

Alilitaka Shirika la Nyumba la Taifa ujenzi wa gharama nafuu uzingatiwe kama ilivyoelezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama tawala kwa kuzifanya ziwe na bei nafuu kwa Watanzania wa kipato cha chini ziwe bora na kuwaletea wananchi maisha bora kwa kupitia nyumba.

"Rais ameshatoa maelekezo kuwa popote NHC inapojenga nyumba pawekewe miundombinu husika na Halmashauri na mamlaka zingine husika kama Tanesco na Maji na ardhi iwepo ya bure na ndiyo maana pale kwenye mradi wa Iyumbu Dodoma, Rais ameahidi kuagiza huduma zitolewe bure.

Alisema anafahamu kuwa NHC inajenga nyumba za biashara iendelee na kasi hiyo bila kuzikwaza zile za gharama nafuu.

"Najua NHC mnajenga nyumba za biashara fanyeni tu ili mradi hampati hasara. Mjikite katika kubuni teknolojia za kisasa zitakazoweza kupunguza gharama. Mjifunze aina mbalimbali za teknoljia. Jengeni mahusiano na idara mbalimbali za serikali. Tumewapa status kama Master Developers ili muwe champion wa upangaji wa miji  fanyeni hivyo tofauti ionekane,"alisema.

Alilitaka Shirika lianzishe kitengo cha kupanga na kupima Ardhi ili kupunguza ujenzi holela na kuiagiza NHC kujenga Miradi midogo midogo yenyewe kwani Kama Shirika ni Mkandarasi wa Daraja la Kwanza "Jengeni wenyewe ili muwe mfano bora kwa makandarasi. Ningependa Bodi mlifanye Shirika liwe stable kwa kuweka ubunifu wenu."

Aliongeza kwa kuitaka Bodi hiyo mpya ijihusishe na usikilizaji wa malalamiko na migogoro yote ya wapangaji kwa kuzingatia sheria zilizopo.


Bodi hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake Mama Blandina Salome Joseph Nyoni na wajumbe   Prof. John M. Lupala, Gabriel Malata, Mary Mlay, Subira Mchumo, Ally Hussein Laay, Pius Maneno na Injinia Kesogukwele Masudi Issa Miraji Msita.
Post a Comment