Sunday, April 30, 2017

JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOSOMA BEIJING WAADHIMISHA MIAKA 53 YA MUUNGANO


Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania wanaosoma Beijing Nchini Husein Mtoro ( katikati) aliyemwakilisha Balozi,aliambatana na Viongozi wote Wakuu akiwemo Makam Mwenyekiti Khamis Ngwali,Katibu Mkuu Ndugu Remidius Emmanuel,Naibu Katibu Mkuu Ndugu Alinanuswe Mwakiluma na Mweka Hazina Ndugu Kulwa Gamba.
Pamoja nao,Viongozi waasisi wa Umoja huo Ndugu Suleiman Serera na Irenius Kagashe nao walishiriki sambamba na Viongozi wastaafu wengine akiwemo Makam Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Kassim Jape,Katibu Mkuu Mstaafu Angelina Makoye,Mtunza Hazina Mstaafu Lusekelo Gwassa katika maadhimisho ya muungano yaliyofanyika mapema wiki hii kwa kushriki maonesho ya utalii na utamaduni. 
Baadhi ya watanzania wanaosoma katika chuo cha Beijing nchini China wakiwa katika maonesho ya utamaduni na utalii kama moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania mapema wiki hii. 
Wadau wakipozi kwa picha 
Maonesho ya utalii na utamaduni yakiendelea Jijini Beijing 


Mmoja wa watanzania anayesoma Beijing akipamba maonesho hayo kwa bendera ya Tanzania wakati wa maonesho ya utalii na utamaduni ikiwa ni maadhimisho ya miaka 53 ya Mungano Hafla hizo zilifanyika mapemaa wiki hii. 
Picha ya pamoja
Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania wanaosoma nchini China,wameadhimisha kumbukumbu ya Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kushiriki MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NA UTAMADUNI katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Biashara na Uchumi jijini Beijing.
Akizungumza kwa niaba ya Balozi wa Tanzania nchini China Balozi MBELWA KAIRUKI,Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,ndugu HUSSEIN MTORO aliwaasa Watanzania hao kudumisha Amani,Mshikamano na kushiriki katika ajenda muhimu za Taifa ikiwemo,kushiriki katika kukuza soko la Utalii kwa kutangaza Vivutio vya asili vya nchi yetu,kuhamasisha Watalii wengi wa kimataifa kutembelea vivutio mbali mbali vilivyopo Tanzania.Pia Mwenyekiti alifikisha salam za Balozi Mbelwa za kuwatakia kila la heri Wanafunzi wote walio katika hatua mbalimbali za kukamilisha Tafiti zao kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.

No comments: