RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI MGENI RASMI UZINDUZI WA RELI YA KISASA

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akioneshwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema   maandalizi ya uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa reli ya kisasa Standard Gauge Pugu jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  akipata maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Reli Tanzania (TRL),  Mhandisi ,Massanja Madogosa  juu ya katika maandalizi ya a uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa reli ya kisasa Standard Gauge Pugu jijini Dar es Salaam.
 .Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa maelekezo  kwa watendaji walipotembelea  maandalizi ya uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa reli ya kisasa 'Standard Gauge' leo Pugu jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Mhandisi Massanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari juu  ya uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa reli ya kisasa utaofanyika leo Pugu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia eneo hilo la tukio hapo.

RAIS Dk. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa  uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi reli ya kisasa itakayofanyika  leo Pugu, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika sehemu ya uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa watanzania waunge mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Amesema reli hiyo ni ya kisasa ambayo itarahisisha usafiri wananchi kuondokana na adha ya kusafiri kwa muda mrefu.Makonda amesema baada ya uzinduzi ajira zitatoka katika ujenzi wa reli hiyo na kuwataka wataopata ajira kuwa walinzi reli hiyo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli (TRL)  Mhandisi Massanya Kadogosa amesema kuwa ujenzi huo utaanza kwa awamu .Amesema miundombinu hiyo hiyo ikikamilika gari moshi litatembea kilomita 160 kwa sasa hivyo kwa safari zote zitakuwa ni fupi na wananchi wanaweza kujenga uchumi.

Comments