BODI YA ZABUNI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAIPA WIKI TANO KAMPUNI YA UJENZI YA KOBERG KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAMISHNA WA UHAMIAJI, JIJINI D’SALAAM
Mwenyekiti wa Bodi ya
Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na
Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (watatu kushoto), Katibu wa Bodi hiyo ambaye
pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi wakimsikiliza Mkuu
wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani (kushoto), wakati
wajumbe wa Bodi hiyo walipotembelea nyumba za makazi za Makamishna wa Uhamiaji,
Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Bodi hiyo ilitoa wiki tano kwa Kampuni ya
Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Katibu wa Bodi ya
Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mkurugenzi wa Manunuzi wa
Wizara hiyo, David Mwangosi akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya
Wizara hiyo, wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba
za makazi ya makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es
Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni ya
Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi
hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na
Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (kushoto) akiangalia kabati la nguo katika
moja ya chumba cha nyumba za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi,
jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi hiyo walizikagua nyumba hizo na kutoa
wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Kitengo cha
Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani akiwaonyesha Wajumbe wa Bodi ya
Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, nyumba za makazi za makamishna wa
Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa
Magereza, Gaston Sanga. Wapili kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi, watatu kulia ni Kamishna wa Fedha
na Utawala wa Uhamiaji, Peter Chogero, na kulia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Edwin Makene. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mhandisi wa Kampuni ya
Ujenzi ya Koberg ambayo inajenga nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya
Uhamiaji, Leonard Leonidace, akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, walipozitembelea nyumba hizo wakikagua maendeleo ya
ujenzi wa nyumba hizo, hata hivyo Wajumbe wa Bodi walitoa wiki kwa Kampuni hiyo
kukamilisha ujenzi. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara hiyo ambaye
pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga, na wanne kulia
ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo,
David Mwangosi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na
Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (Katikati) na Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia
ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi (wanne kulia), wakiwa
katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo, mara baada ya wajumbe hao
kumaliza ziara yao ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi za Makamishna wa Idara
ya Uhamiaji, zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe
wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo.
Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
IMEANDALIWA NA KITENGO
CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA
NDANI YA NCHI
&&&&&&&&
Bodi ya Zabuni ya Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, imeipa muda wa wiki tano Kampuni ya Ujenzi ya Koberg Construction Co.Ltd kukamilisha ujenzi wa nyumba za makazi
za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji hapa nchini zilizoko katika eneo la Mtoni Kijichi
jijini Dar es Salaam ambazo zitatumiwa na Makamishna hao.
Uamuzi wa Bodi hiyo umekuja
baada ya Kampuni ya Koberg
Construction ya nchini hapa kuonyesha
kusuasua na kushindwa kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo kwa wakati.
Bodi hiyo inayoongozwa na
Mwenyekiti wake Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga
na Katibu wake Bw. David Mwangosi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha
Manunuzi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imefanya maamuzi hayo baada ya
kufanya ukaguzi na kujionea hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba hizo.
Kwa upande wake Katibu wa
Bodi hiyo amesema kitendo cha Mkandarasi huyo kusuasua kukamilisha kwa wakati
kazi ya ujenzi wa nyumba hizo ulioanza tangu mwaka wa Fedha wa 2014/2015 ndicho
kilichoifanya Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo
kuamua kutembelea eneo ambalo kazi ya ujenzi wa nyumba hizo unaendelea na kumpatia
wiki tano tu kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo.
Comments