Sunday, April 09, 2017

NAIBU WAZIRI MASAUNI AONGOZA BONANZA LA VIKUNDI VYA MICHEZO, VIWANJA VYA JWTZ, VISIWANI ZANZIBAR

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) akifanya mazoezi na vikundi vya michezo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara kabla ya kufungua Bonanza kubwa la michezo lililofanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wanamichezo hao pamoja na wananchi hapa nchini kwa ujumla, kudumisha mazoezi zaidi ili waweza kupata afya bora.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wanamichezo wa vikundi mbalimbali kutoka Zanzibar na Tanzania Bara mara baada kiongozi huyo kufanya mazoezi ya viungo na wanamichezo hao katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wanamichezo hao pamoja na wananchi hapa nchini kwa ujumla, kudumisha mazoezi zaidi ili waweza kupata afya bora.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani

Msoma Risala wa Kikundi cha Michezo cha Island Erercise Club cha mjini Unguja, Zanzibar, Ally Mussa, ambacho ndio waratibu wa Bonanza la Vikundi vya Michezo kutoka Visiwani humo pamoja na Tanzania Bara, akitoa historia fupi ya kikundi hicho pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, kabla ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kukariboishwa kuzungumza na mamia ya wanamichezo ambao walifanya mazoezi mbalimbali katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar leo.  Wapili kulia ni Bregedi Kamanda KV101 kambi ya nyuki, Kanali Fadhili Nonda. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiumwagilia maji mti wa kumbukumbu alioupanda katika eneo la Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar, mara baada ya kufanya mazoezi ya viungo katika Bonanza la Vikundi vya Michezo kutoka visiwani humo pamoja na Tanzania Bara. Masauni aliwakilisha Makamu wa Rais, Sami Suluhu katika sherehe hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Post a Comment