Kufuatia uteuzi wa Bibi Blandina S.J. Nyoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 25/02/2017. Mhe. William V. Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(2) cha Sheria Na. 2 ya Mwaka 1990, amewateua Wajumbe 7 wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa.
Aidha, uteuzi huu ni wa kipindi cha miaka mitatu (3), kuanzia tarehe 23 Machi, 2017.
Majina ya wajumbe hao ni kama ifuatavyo:
- Prof. John M. Lupala
- Bwn. Gabriel Malata
- Bi. Mary Mlay
- Bi. Subira Mchumo
- Bwn. Ally Hussein Laay
- Bwn. Pius Maneno
- Bwn. Kesogukwele Masudi Issa Miraji Msita
Imetolewa na:
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Comments