Monday, April 24, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MAELEZO ONLINE TV MJINI DODOMA

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe,Naibu Waziri wake Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas wakifurahi mara baada ya kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akibonyeza kitufe kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.Televisheni iyo itaonyesha kazi mbalimbali za Wizara,Taasisi na Idara za Serikali.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Anastazia Wambura.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akiangalia mahojiano yaliyofanyika kati ya Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo Hassan Abbas na Makamu wa Rais Mhe.Samia Hassan Suluhu kuhusu maadhimisho ya Muungano yatakayofanyika mjini Dodoma.Mahojiano hayo ni ya kwanza kupitia televisheni ya mtandaoni ya Idara ya habari-MAELEZO.

Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Harrison  Mwakyembe akizungumza na menejimenti ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo(Hawapo Pichani) na kuipongeza Idara ya habari kwa kuwa wabunifu.Kulia kwake ni Naibu Waziri wake Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA.


Na Daudi Manongi-MAELEZO.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe ameipongeza Idara ya Habari-MAELEZO kwa ubunifu mkubwa  katika kuitangaza Serikali. ameyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akizindua televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO inayoitwa MAELEZOTV.

“Napenda nichukue fursa hii kwa kuwapongeza Idara ya Habari kwa kazi nzuri mnayoifanya katika Wizara hii,nawapongeza kwa ubunifu mkubwa na leo tunazindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara hii  kwa mara ya kwanza katika historia ya Wizara yetu na Idara ya Maelezo kwa ujumla kuwa na” Alisema Waziri Mwakyembe.

Amesema kuwa kwa kazi ya kwanza ambayo imeonekana katika televisheni hiyo imeonyesha weledi wa hali ya juu na kuwataka viongozi wengine wa Wizara hiyo kuiga mfano mzuri na kuwa wabunifu na kusisitiza kuwa nchi yetu ina vipaji na ubunifu wa hali ya juu ikiwemo timu yetu ya Vijana ya Serengeti Boys na n.k

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO,amesema  kuanzishwa kwa televisheni hii ya mtandaoni itasaidia kwa kiasi kikubwa Serikali katika kutangaza matamko mbalimbali na uzinduzi wake wa mapema utasaidia kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii husika.

“Sisi kama Serikali tumekuwa makini katika kuimarisha mawasiliano kati yetu na wananchi na hii televisheni ya mtandaoni itatusaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha dhima ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza kazi zake”,Aliongeza Dkt Abbas.

Mbali na hayo amesema kuwa kipindi cha kwanza kabisa kuwekwa katika televisheni hii itakuwa mahojiano ya maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya muungano  waliyofanya na Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano Mhe.Samia Hassan Suluhu.
Post a Comment