MSANII ROMA MKATOLIKI AZUNGUMZIA SAKATA LA KUTEKWA KWAKE NA WASANII WENZAKE, AONGOZANA NA WAZIRI MWAKYEMBE



.Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake pamoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe Records iliyopo Masaki jijini Dar es salaam, Roma ameiomba serikali kuwahakikishia ulinzi wasanii pamoja na watanzania kwa ujumla kwakuwa inaonesha hawana usalama kabisa kutokana na tukio lenyewe lilivyowatokea , kushoto ni Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe 
Roma Mkatoliki akifafanua zaidi kwa waandishi wa Habari

Roma akiwaonesha wana habari namna alivyojeruhiwa aliokuwa akiteswa na hao watekaji ambao mpaka sasa hawajajulikana ni akina nani,kufuatia Uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akimsikiliza kulia Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake paoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es salaam, Roma ameiomba serikali kuwahakikishia ulinzi wasanii pamoja na watanzania kwa ujula kwakuwa inaoyesha hawana usalama kabisa kutokana na tukio lenyewe lilivyowatokea , kushoto ni Mkewa wa Msanii huyo Bi Nancy.

Baadhi ya Wana Habari wakimsubiri msanii wa Muziki wa Kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Roma Mkatoliki kuja kuzungumza nao na kuwaeleza kilichowatokea

Baadhi ya Wana habari wakifuatilia tukio hilo 
Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akimsikiliza kulia Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake paoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es salaam


Mke wa Roma Mkatoliki pamoja na baadhi ya wasanii wakisubiri kuanza kwa mkutano huo wakati Msanii huyo akijiandaa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la kutekwa kwake kulia ni Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe. 
Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akiongozana na wasanii Roma Mkatoliki na wenzake ili kuzungumzia sakata la Roma Mkatoliki lililotokea hivi karibuni.


Comments