Wednesday, September 28, 2011

Kampeni za helikopta Igunga za nini??

Helkopta ya itakayotumiwa na mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) ikiwasili katika uwanja wa Barafu uliopo Igunga Mjini kwa ajili ya kampeni za mgombea ubunge katika jimbo hilo jana.

Helikopta iliyokodishwa Chadema, ikipita juu ya Anga ya Igunga baada ya kuwasili jana alasili kwa ajili ya mikutano ya mwisho ya kampeni ya chama hicho.
Helikopta ya iliyokodishwa na CCM ikitua katika uwanja wa Sabasaba mjini Igunga jana kwa ajili ya kampeni za mwisho za chama hicho.
Hivi resources zote hizi zinazotumika kukampeni huko jimbonio Igunga zingetumika kununulia madawa, kusaidia elimu, barabara na kadhalika katika kipindi cha kabla na baada ya kampeni si ingekuwa ni bora zaidi kuliko ilivyo sasa, hivi wananchi wa Igunga wanahitaji helikopta kweli, je wananchi wa Igunga ni washamba kiasi hicho?
Ni kweli baadhi ya maeneo yapo mbali sana na si rahisi kuyafikia,lakini maswali ni mengi mno kuliko majibu. Ujio wa helikota hizi unaonyesha kuna tatizo kubwa sana la kisiasa na kijamii nchi mwetu. Uongozi unatafutwa kwa fedha nyingi sana mpaka inatisha.

2 comments:

nyahbingi worrior. said...

Habari za siku.
Kama mwanablogu kutoka Tanzania,nakuomba kushiriki kuchangia Mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).

Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya
http://blogutanzania.blogspot.com/
kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.
Ahsante
Luiham Ringo.

Anonymous said...

jamani tusioneshane ufahari wakati mambo muhimu yanayowakabili wananchi tunashindwa kuyatatua,tutaona helikopta mashangingi lakini mkishapata kura kesho tuko wenyewe,maji hakuna,umeme hakuna,hospitali hatuna uwezo wa kulipia matibabu,madarasa hayana madawati!