Soko la Mwanjelwa-2 lateketea kwa moto





SOKO la Sido lililojengwa na kutumika baada ya kuungua moto kwa Soko kuu la Mwanjelwa jijini Mbeya mwaka 2006, nalo limeteketea kwa moto, kujeruhi watu 20 na kusababisha upotevu mkubwa mali.

Tukio hilo lililosababisha vilio, simanzi na hofu kwa wafanyabishara sokoni hapo limekuja takriban miaka minne na nusu tangu soko la Mwanjelwa liungue moto Desemba, 2006.

Habari zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 3 asubuhi baada ya eneo la katikati ya soko kulipuka na kuwaka moto katika kipindi ambacho tayari wafanya biashara wameanza kufungua bidhaa zao.

Mashuhuda wa tukio hilo waliklieleza gazeti hili kuwa waliona moto huo katikati ya soko na wafanyabiashara wakijitahidi kuuzima bila mafanikio.

“Kwa kweli moto ni mkubwa na hatujui chanzo chake nini kwani ghafla tumeona moto ukiwaka eneo la soko upande wa katikatika wa soko hilo hivyo kila mtu anashangaa ulikoanzia moto huu,”alisema mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Francis James

Alisema kuwa magari ya zimamoto ya halmashauri ya jiji la mbeya yamefika eneo la tukio lakini yameshindwa kuuzima moto huo baada ya kuonesha kuongezeka kwa kasi kuwa mkubwa na badala yake wananchi kufanya juhudi ya kuokoa mali zao.

“Kwa sasa tayari jeshi la polisi limefika hapa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kuokoa mali zao ikiwa ni pamoja na kuzuia vibaka kuiba mali za watu kwani hali ni mbaya wafanyabiashara na wananchi wengi wamechanginikiwa kutokana na magari hayo kushindwa kuzima moto huo,”alisema

Akizungumza na Mwanachi Katibu wa soko kuu la zamani la Mwanjelwa Godfrey Haule alisema kuwa uwezekano wa kuuzima moto ni mgumu kutokana na moto kuendelea kuongezeka kwa kasi na kwamba gari la zimamoto limeondoka eneo la tukio baada ya kuishiwa maji na kwenda kuongeza maji.

Haule alisema kuwa moto huo ulianza kuwaka katika ya soko katika vibanda vya wakina mama lishe (mama ntilie) ambapo moto huo ungeweza kuzimwa mapema lakini walishindwa kufanya hivyo kutokana na kukosa maji kwa sababu mabomba ya yaliyopo katika soko hilo hayatoi maji na hivyo kusubiria magari ya ziamoto ambayo pia yameshindwa kuuzima moto huo.

“Mabomba ya soko yangekuwa yanatio maji tungefanikiwa kuuzima moto mapema lakini tulishindwa baada ya kwenda kungulia mabomba hayo yakakawa hayatoki maji na lilikuja hapa gari la zimamoto pia limeshindwa kuuzima moto huo kutokana na kuwa mkubwa walivhoambulia na kiushiwa maji katioka gari na kwenda kuongeza mengine,”alisema

Comments