Maafa ya Zanzibar

Katibu Mkuu kiongozi Philemon Luhanjo akitoa tamko la serikali kuhusiana na ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea mwishoni mwa wiki.
Rais Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akitoa salamu zake za pole mara baada ya kumalizikia kwa dua ya pamoja iliyokuwa maalumu kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya meli iliyotokea Unguja mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wakiswali wkati wa dua maalumu ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea mwishoni mwa wiki eneo la Nungwi, Unguja. Swala hiyo ya pamoja ilifanyika jana Septemba 12 katika viwanja vya Maisara.
Balozi wa Marekani nchi Tanzania Alfonso Leinhardt akimfariji Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia ajali ya meli ya Spice Islanders iliyotokea huko Nungwi, Unguja juzi usiku ambapo watu zaidi 200 wamepoteza maisha na wengine 602 kuokolewa wakiwa hai.Picha na Freddy Maro
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji na kuwapongeza wananchi wa kijiji cha Nungwi kufuatia juhudi zao za kujitolea kuwaokoa watu waliopata ajali katika meli ya MV Spice Islanders iliyotokea juzi usiku.Meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kwenda Pemba amapo watu zaidi ya 200 wanahofiwa kufa maji.

Comments