Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiasalimiana na baadhi ya Watanzania waliohudhuria ibada maalumu ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Kanisa Katoliki ya Mashahidi wafia dini wa Uganda huko eneo la Namugongo,nje kidogo ya jiji la Kampala(picha na Freddy Maro)
Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Rais Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya ibada maalumu kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa la Mashahidi wafia dini wa Uganda huko eneo la Namugongo, nje kidogo ya jiji la Kampala leo asubuhi.Wa kwanza kushoto ni Askofu Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba na wapili kushoto ni Dr.Cyprian Lwanga Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Kanisa Katoliki Kampala.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiagana na Mama Maria Nyerere muda mfupi baada ya kumalizika kwa misa Maalumu ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili atangazwe kuwa Mwenye Heri iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mashahidi wa Uganda huko Namugongo, nje kidogo ya mji wa Kampala leo asubuhi.Misa hiyo iliyohudhuriwa pia na baadhi ya waumini kutoka Tanzania ni sehemu ya mchakato ilioanzishwa na kanisa Katoliki Tanzania wenye nia ya kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa Mwenyeheri na hatimaye Mtakatifu kulingana na vigezo na kanuni zilizowekwa na Kanisa hilo.
Comments