Monday, June 21, 2010

safari za treni reli ya kati zaanza




KAMPUNI ya Reli nchini (TRL) imezindua rasmi safari moja kwa wiki ya treni ya abiria badala ya tatu kama ilivyo zoeleka.

Safari hizo zilizinduliwa jana baada ya kusitishwa kwa miezi sita kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha sehemu mbalimbali za nchini na kusomba daraja na reli za Kampuni hiyo.

Akizungumza na Mwananchi katika Makao Makuu ya TRL muda mfupi kabla ya kuzindua safari hiyo kwa kupeperusha bendera yenye rangi ya kijani, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Hundi Chaudhary alisema kwa sasa wanaanza na safari za Kigoma.

“Kwa sasa tunanza na safari za kigomo pekee kwa sababu hatuna mabehewa ya kutosha na safari hii itakuwa ikifanyika mara moja kwa wiki ambayo ni kila Ijimaa,”alisema Chaudhary.

Alisema treni hiyo imeondoka na mabehewa 15 badala ya 21 ikiwa na abiria 600 tu kwa ajili ya abiria wa Kigoma ambao wanapata shida kutoka na mkoa huo kukosa miundombinu sahii kwa usafiri wa basi.

Kuhusu usalama wa treni hiyo ambayo imemaliza miezi sita bila ya kufanyakazi kiasi cha kusababisha mabehewa sita kushindwa kufanya kazi kutokana na ubovu Chaudhary alisema, kuna usalama wa kutosha na abiria wote watafika salama.

“Hii treni inausalama wa kutosha na mafundi wetu pamoja na watalaam kutoka Mamla ya Udhibiti wa Safari za Majini na nchi kavu (Sumatra) wameikagua na kuridhika na matengenezo madomadogo yaliyofanywa kabla ya safari hiyo kuanza,”alisema Chaudhary.

Wakati Mkurugenzi huyo akisema hayo baadhi ya abiria waliosafiri na treni hiyo jana walisema kurejea kwa safari hiyo imewasaidia na itaendelea kuwasaidia kwa sababu ni miezi sita sasa wamekuwa wakisafiri kwa shida.

“Safari hii ilivyonza leo imetusaidia sana kwa sababu sisi wananchi wa Kigoma tumesaulika kwa kipindi kirefu ndani ya nchi hii na tunapata shida kila siku,”alisema Amina Saidi.

Saidi alisema, tangu safari za treni hiyo zilipositishwa hajawai kusafiri kwenda Kigoma kutoka na shida ya usafiri na kwamba alishakata tamaa ya kufasiri kwa sababu hana uwezo wa kwenda Kigoma kwa usafiri wa basi. Picha na taarifa za Jackson Odoyo. SOURCE: MWANANCHI.

1 comment:

Anonymous said...

ukiangalia hapa inaonyesha wabongo tunaweza kujisaidia wenyewe, kama sikosei wamesema madaraja yamekarabatiwa na jeshi letu, hii ni dalili nzuri, hatuhitaji kuomba msaada kila mara.