ZAIDI ya kaya 89 hazina makazi baada ya nyumba zao kubomolewa katika maeneo ya Kibamba mji mpya kwa amri ya mahakama ya Kinondoni.
Wakizungumza na Mwananchi mwishoni mwa wiki jijni Dar es Salaam waathirika wa bomoabomoa hiyo waliopo hapo juu pichani wakiwa katika vibanda baada ya kubomolewa nyumba zao walidai kuwa hawajawahi kuambiwa chochote juu yao kuishi katika eneo hilo.
“Tumeishi hapa kwa miaka minne sasa na hatujawa kusikia chochote kuhusu eneo hili wala kuambiwa kuwa ni eneo lenye mgogoro,”alisema Ferster Fumbe.
Alisema kuwa kilichowashangaza zaidi kuhusu suala hilo ni hatua ya watu waliodai kuwa wametumwa na mahakama hiyo kuja na Askari Polisi pamoja na kundi kubwa la wahuni kwa ajili ya kuboa nyumba hizo.
Jumbe alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 7 asubuhi akiwa na wiki mbili tangu alipojifungua mtoto wake wa kiume kwa njia upasuaji na kwamba ghafla akashtukia kundi kubwa la watu kunvamia na kunaza kuboa nyumba yake huku baadhi yao wakichukua vitu ndani. Jackson Odoyo: Source MWANANCHI.
Comments