Sunday, January 11, 2009

watu 27 wafariki dunia Tanga



MJI wa Tanga na maeneo mengine ya jirani, jana yalizizima kwa majonzi yaliyotokana na ajali ya basi la Kampuni ya Tashriff, iliyosababisha watu 27 kufa papo hapo na wengine 23 kujeruhiwa.

Ajali hiyo ilitokea saa 2.30 usiku wa juzi, katika eneo la mji mdogo wa Hale wilayani Korogwe, barabara kuu ya Segera-Tanga.

Habari zilisema majeruhi za wawili wa ajali hizo ni mbaya mno na wamelazwa katika Hospitali ya Teule ya Muheza.

Kwa mujibu wa habari hizo, ajali hiyo ilitokea wakati basi hilo likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Tanga.

Basi hilo aina ya Isuzu, lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina
moja tu la Mdoe au kwa kwa jina la utani la Osama.

Inasemekana katika ajali hiyo, basi hilo, lililivaa kwa upande wa kushoto, lori lililokuwa limeba magogo na kuegeshwa kandakando mwa mwa barabara.

Kwa mujibu wa maelezo ya watu walioshuhudia, magogo hayo yaliwakumba abiria waliokuwa wameketi kuanzia kiti cha kwanza hadi cha mwisho katika basi la Tashriff na baadhi ya abiria waliokuwa wamesimama tayari kwa kushuka katika kituo cha Hale.

No comments: