Monday, January 26, 2009

mambo yamebadilika

HEBU cheki mvua inavyofanya mambo hapa ni katikati ya jiji leo mchana ni Kariakoo karibu na shule ya Uhuru ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema mvua zinazonyesha sasa katika ukanda wa Pwani sio za vuli bali ni za mda mfupi na zitaishi hivi karibuni..

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Philbert Tibaijuka, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa mvua hizo zitaisha kesho.

“Hali hii siyo ya kudumu itachukua takriban siku tatu, hivyo ningependa wananchi watambue kuwa hizi siyo mvua za msimu wala vuli,” alisema Tibaijuka na kubainisha kuwa hali hiyo hutokea kila mwaka katika ukanda wa Pwani na Maziwa Januari na Februari.

Alisema mvua hizo zimesababishwa na matukio mbalimbali ikiwamo mfumo unaoandamana na mfumuko wa hali ya hewa unaosababisha upande mmoja wa pepo za Kaskazini Mashariki kukosa nguvu.
“Kumekuwepo na upungufu wa mgandamizo wa hali ya hewa kuanzia Arabia mpaka kaskazini mwa Bahari ya Hindi hali ambayo imesababisha kupungua kwa upepo katika maeneo hayo na mvua kufanyika katika eneo ambalo ni jirani na mwambao wa Pwani ya Tanzania,” alisema

No comments: