Tuesday, January 13, 2009

hali mbaya mafuta



Mafuta yameadimika kwenye vituo vingi jijini Dar es Salaam tangu mwishoni mwa wiki, ikiwa ni siku chache baada ya mamlaka inayohusika na nishati hiyo, Ewura kutangaza bei elekezi ambayo ni chini ya bei iliyokuwa inatumiwa na wauzaji wa mafuta.

Ewura ailitangaza kuwa mafuta aina ya petroli yauzwe hadi Sh1,166 kwa lita na dizeli iuzwe kwa Sh1,271 kwa lita tofauti na bei za awali za Sh1,450 hadi Sh1,600 kwa lita ya petroli na Sh1,300 hadi Sh1,500 kwa lita ya dizeli. Bei hiyo elekezi ndiyo iliyozua kasheshe tofauti, ikiwa ni pamoja na upungufu wa ghafla.

Kutokana na agizo hilo wafanyabiashara wa mafuta huenda wanafanya uharamia na sasa hali imezidi kuwa mbaya jana wakati vituo vingi zaidi vipositisha huduma hiyo na kusababisha kuwepo kwa misululu mirefu kwenye vituo vilivyokuwa vikiuza na hasa kituo cha BigBon kilicho Kariakoo, ambako magari yalipanga mstari mrefu iliyokuwa pembeni ya mistari ya watu waliobeba madumu.

Sehemu nyingine ambako mafuta yalikuwa yakiuzwa ni kituo cha Gapco kilicho Victoria, Mikocheni na vituo vya Engen. Vituo vya Gapco (Banana Ukonga), Oilcom (Ukonga Madafu), Oilcom (Mzambarauni), BP (Uwanja wa Ndege) na vingine vingi vilivyo wilayani Ilala havikuwa na huduma hiyo.


No comments: